CURRENT NEWS

KITAIFA

Siasa

MICHEZO NA BURUDANI

Monday, February 19, 2018

MHE BITEKO AAGIZA NDANI YA WIKI MBILI KUFUNGULIWA MGODI WA NYAKAVANGALA MKOANI IRINGA

Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018.
Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisikiliza maelezo mbalimbali kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ,mara baada ya kuwasili katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018.
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Mkoani Iringa wakinasa kumbukumbu muhimu kwa ajili ya kuhabarisha wananchi juu ya ziara ya Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko mkoani humoLeo 19 Februari 2018.
Umati mkubwa wa wachimbaji wadogo katika mgodi wa mgodi wa Nyakavangala uliopo katika Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa wakisikiliza hatma ya mgodi huo kutoka kwa Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika Leo 19 Februari 2018.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko aakikagua mashimo mbalimbali kabla ya kuzungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara katika mgodi wa Nyakavangala uliopo Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa, Leo 19 Februari 2018. 

Na Mathias Canal, Iringa

Naibu Waziri Wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameagiza kufunguliwa ndani ya wiki mbili mgodi wa Nyakavangala uliopo katika Kata ya Malengamakali Wilaya na Mkoa Wa Iringa ili kuwarahisishia huduma wachimbaji wadogo za kujiingizia kipato chao.

Mhe Biteko ameyasema hayo Leo 19 Februari 2018 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano Wa hadhara Mara baada ya kuwasili mgodini hapo kukagua hatua za kiusalama zilizofikiwa tangu kufungwa kwa mgodi huo 12 Februari 2018 kufuatia matukio matatu ya ajali ambayo yalipelekea vifo vya wachimbaji wanne.

Mhe Biteko akiwa ameambatana na Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa Mhe Amina Masenza, Kamati za ulinzi na usalama Wilaya na Mkoa wa Iringa, Mkuu Wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela na wataalamu Wa Madini kutoka Wizara ya Madini ameagiza kuchukuliwa hatua za haraka za kujiridhisha uhakika Wa usalama Wa wachimbaji kuanzia Leo 19 Februari 2018 hadi kufikia 5 Februari 2018 mgodi uwe umeanza uchimbaji.

Alisema kuwa kufunguliwa kwa mgodi huo kutaongeza kipato cha wachimbaji hao huku akisisitiza wachimbaji hao pindi mgodi utakapofunguliwa kuzingatia taratibu za usalama mgodini na kulipa kodi stahiki za serikali.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia kuwanufaisha wananchi kupitia rasilimali zao ikiwemo Madini ambapo Tanzania ni nchi yenye fursa nyingi kwa uchimbaji Madini ilihali wananchi hawanufaiki ipasavyo na rasilimali hiyo.

Mhe Rais Magufuli ametuagiza kuwalea na kuwasimamia wachimbaji wadogo nchini ili kutoka kwenye uchimbaji mdogo na kuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa ili uchumi wa nchi ushikwe na watanzania wenyewe.

Alisema kuwa wachimbaji hao wanapaswa kushirikiana na serikali kuwafichua waovu wanaoiibia serikali rasilimali Madini kwa kuyatorosha kwenda sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi pasina kulipa kodi.

"Jichungeni na kujilinda wenyewe ili kila kinachopatikana serikali ijue imepata kiasi gani na wachimbaji wameingiza kiasi gani na kisemwe hadharani, ndugu zangu Rais anahangaika kuona kila eneo ambalo lina wachimbaji wadogo wana rasimishwa na hatimaye wananufaika na madini yao, lakini bado kuna watu wanatorosha madini" Aliongea kwa msisitizo Mhe Biteko na kuongeza kuwa

"Na Mimi nataka niwaambieni wale wote wanaofikiri katika serikali hii inayoongozwa na Rais Magufuli wanaweza kupenya na dhahabu watafute jambo jingine la kufanya maana jambo hilo limepitwa na wakati"

Alisisitiza kuwa wamiliki wa leseni kote nchini wanapaswa kutunza kumbukumbu za biashara nzima ya madini ikiwemo mapato na matumizi kwa muda usiopungua miaka mitano kinyume na hapo kwa mujibu wa sheria watatozwa faini ama kifungo jela

Kwa upande wake Mhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza alisema kuwa wachimbaji hao wanapaswa kutofanya kazi kwa mazoea huku akisisitiza wachimbaji hao kuwa na ushirikiano na kupendana.

Sambamba na hayo pia aliwasihi kuwa makini na kutofanya ngono zembe kwani matokeo yake ni kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI jambo litakalopelekea kupoteza nguvu kazi katika familia na Taifa kwa ujumla.

MWISHO

RAIS WA FIFA KUFANYA MAJADILIANO NA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZONa Anitha Jonas – WHUSM

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Duniani (FIFA) kufanya mkutano wa majadiliano na vyombo vya habari kumi na mbili vya ndani ya nchi.
Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika mkutano na wahariri wa habari za michezo uliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
‘’Huu ni utaratibu wa viongozi wa FIFA kufanya mkutano wa mazungumzo na waandishi wa vyombo vya habari katika nchi wanazofanyia mikutano yao  ya kikazi kama ulivyo mkutano huu wanaotarajia kuufanya nchini Februari 22,mwaka huu,’’alisema Dkt. Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Waziri Mwakyembe alieleza kuwa Rais wa FIFA Bw. Gianni Infantino anatarajia kuwasili nchini alfajiri ya saa nane usiku kuamkia Februari, 22 2018 ambayo ndiyo siku ya mkutano na saa tatu asubuhi yake ataelekea ikulu kukutana na viongozi wakuu wa nchi.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Bw.Wilfred Kidau alitoa ufafanuzi kuhusu mkutano huu wa viongozi wa FIFA na CAF kuwa umebeba ajenda mbalimbali  ikiwemo kujadili kuhusu Maendeleo ya Soka la Wanawake,Maendeleo ya Soka la Vijana,Utaratibu wa kusaidia Vilabu vya soka pamoja na vipaumbele mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.
‘’Mkutano huu wa FIFA unatarajia kufanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam (JNICC) na ni sawa na kikao cha ndani ambacho kimelenga zaidi kujadili masuala ya maendeleo ya shirikisho hilo kwa ajili ya kuandaa agenda za mkutano mkuu wa FIFA wa dunia hivyo ombi kwa waandishi wa habari ni kuelewa dhana ya mkutano siyo kuwa wamenyimwa fursa bali huo ndiyo utaratibu’,’alisema Bw. Kidau.
Pamoja na hayo Bw.Kidau alifafanua kuwa miongoni mwa vyombo vitakavyopata fursa ya kushiriki majadiliano hayo baadhi yao watarusha mazungumzo hayo mbashara katika vyombo vyao hivyo wadau wengine wataweza kufuatilia tukio hilo moja kwa moja kupitia vyombo hivyo.
Halikadhalika Rais huyo wa FIFA anatarajia kuondoka nchini jioni mara baada ya kumaliza mkutano mwake na kushiriki chakula cha jioni.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi wa idadi ya waandishi watakaohitajika katika mkutano wakati wa mkutano wa  majadiliano na Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) Bw.Gianni Infantino utakaofanyika mnamo Februari 22, Mwaka huu na waandishi wa habari, katika mkutano wake na Wahariri wa Habari za Michezo (hawapo pichani) nchini leo jijini Dar es Salaam,Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Suzan Mlawi na Kulia ni Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wilfred Kidau .
 Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw.Wilfred Kidau akitoa ufafanuzi kuhusu ajenda za mkutano wa Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) na CAF utakaofanyika nchini Februari 22,2018 katika mkutano na  Wahariri wa Habari za Michezo nchini  (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari kutoka Gazeti la Nipashe Bi Somoe Ng’itu akiuliza swali kuhusu utaratibu wa waandishi wa habari watakaofika Ikulu kuripoti tukio la Rais wa Shirikisho la Mipira wa Miguu Duniani (FIFA) kukutana na viongozi wakuu wanchi, kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani ) leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wahariri wa habari za michezo nchini.
  

DKT.KIGWANGALLA AITEMBELEA FAMILIA YA AKWILINA, ATOA UBANI WA POLE


Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo ametembelea nyumbani kwa familia ya Akwilina na kutoa ubani wa pole kwa msiba huo.

"Nimefika hapa kama Raia mwema tu ambaye nimeguswa na msiba huu na nimetafakari kwani na mimi kipindi fulani nilipitia chuo hasa kutoka familia zetu hizi masikini kwa hiyo inapotokea ukio kama ili unaona ni pigo kwa familia, pigo kwa jamii, pigo kwa wanafunzi wenzake na pigo kwa Taifa kwa ujumla wake" alieleza Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na vyombo vya Habari msibani hapo.

Dkt.Kigwanalla ambaye alifika msibani hapo majira ya saa saba mchana, aliweza kuungana pamoja na ndugu na jamaa wa wafiwa ambapo pia alipata chakula cha mchana pamoja na waombolezaji wengine sambamba na kutoa ubani wake kama mwananchi mwingine.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli ambaye yupo hapo kwa ajili ya kusimamia shughuli  kwa upande wa Serikali, amebainisha kuwa wataendelea kuratibu baadhi ya mambo yanayoendelea hapo kwani msiba huo kwa namna moja Serikali imeguswa nao.

Mbali na Mkuu wa Wilaya hiyo, Wengine waliofika hapo ni pamoja na Mkurugenzi wa Ubungo, John Kayombo ambapo kwa pamoja na watendaji wengine wa Kiserikali wameweza kusaidiana na familia ya marehemu katika shughuli mbalimbali zinazoendelea msibani hapo.

Aidha, jana viongozi wengine waandamizi wa Serikali akiwemo Waziri Elimu, Mh. Ndalichako, Naibu Waziri wa Ulinzi Masauni na IGP  Siro waliweza kutembelea kutoa pole katika familia hiyo.

Akwilina kabla ya kifo chake alikuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya chama cha siasa cha CHADEMA. 


KAWAIDA:
Dkt.Kigwangalla aitembelea familia ya Akwilina, Atoa ubani wa pole
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo ametembelea nyumbani kwa familia ya Akwilina na kutoa ubani wa pole kwa msiba huo.
"Nimefika hapa kama Raia mwema tu ambaye nimeguswa na msiba huu na nimetafakari kwani na mimi kipindi fulani nilipitia chuo hasa kutoka familia zetu hizi masikini kwa hiyo inapotokea ukio kama ili unaona ni pigo kwa familia, pigo kwa jamii, pigo kwa wanafunzi wenzake na pigo kwa Taifa kwa ujumla wake" alieleza Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na vyombo vya Habari msibani hapo.
Dkt.Kigwanalla ambaye alifika msibani hapo majira ya saa saba mchana, aliweza kuungana pamoja na ndugu na jamaa wa wafiwa ambapo pia alipata chakula cha mchana pamoja na waombolezaji wengine sambamba na kutoa ubani wake kama mwananchi mwingine.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli ambaye yupo hapo kwa ajili ya kusimamia shughuli  kwa upande wa Serikali, amebainisha kuwa wataendelea kuratibu baadhi ya mambo yanayoendelea hapo kwani msiba huo kwa namna moja Serikali imeguswa nao.
Mbali na Mkuu wa Wilaya hiyo, Wengine waliofika hapo ni pamoja na Mkurugenzi wa Ubungo, John Kayombo ambapo kwa pamoja na watendaji wengine wa Kiserikali wameweza kusaidiana na familia ya marehemu katika shughuli mbalimbali zinazoendelea msibani hapo.
Aidha, jana viongozi wengine waandamizi wa Serikali akiwemo Waziri Elimu, Mh. Ndalichako, Naibu Waziri wa Ulinzi Masauni na IGP  Siro waliweza kutembelea kutoa pole katika familia hiyo.
Akwilina kabla ya kifo chake alikuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya chama cha siasa cha CHADEMA. 
Marehemu Akwilina enzi za uhai wake
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa familia ya Akwilina alipotembelea hapo kutoa pole
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akipata taarifa kutoka kwa ndugu Akwilina amabye alikuwa ni mlezi wa binti huyo.
 
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo
Waombolezaji wakipata chakula cha mchana msibani hapo
Viongozi wa Serikali wakipata chakula msibani hapo
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya ndugu na jamaa walijitokeza katika msiba huo, Mbezi Luis, Jijini Dar e Salaam
  
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio hilo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akizungumza na wanahabari wakati wa tukio hilo
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio hilo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akizungumza na wanahabari wakati wa tukio hilo.

MAGAZETI YA TZ NA NJE LEO FEBRUARY 19,2018

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania