CURRENT NEWS

Sunday, December 9, 2007

Nini maana nzima ya uongozi?(Challenge kwa Watanzania)


Uongozi ni neno lenye maana nyingi na linalochukua dhamana ya watu na vitu vilivyomo, lakini je uongozi ni nini haswa kwa karne hii ya sayansi na teknolojia?
Lakini kuna maana gani kama uongozi unashindwa kufanya kazi ,au kutimiza yale walioahidi,nikiwa na maana kutokuwa na utekelezaji wala miundo mbinu?
Ahadi zilikuwa nyingi sana wakati wa kampeni lakini hakuna kinachoendelea,yaani ni kama moshi wa kifuu!!!
Najua tupo kwenye vugu vugu la uchaguzi yaani mwezi wa nne(April) tunachagua viongozi wapya na nafikiri safari hii tusirudie makosa,maana hata ile kuchagua kimajina na uwezo wakifamilia itabidi viwe kando la sivyo tutarudia yaleyale ya kutwanga maji kwenye kinu.

Tunahitaji kiongozi anayejitolea,anayeajali wananchi wake bila kuwa na tofauti binafsi,anayeshirikiana na watu kuanzia wagonjwa ,viongozi ambao wanatusaidia sisi wanafunzi wa kimataifa kuapata unafuu wa kuishi kwa kuongea na kutafuta udhamini mbalimbali.
Tunahitaji uongozi wenye upendo wa hali ya juu na si huu wa kuonyeshana chuki na kuishi kimakundi makundi,hatukuja hapa kuishi kimakundi ,tumekuja kusoma na hilo ndio lengo.

Cha ajabu uongozi umeshindwa hata kuwakutanisha Watanzania katika kusheherekea siku kuu ya uhuru,ambapo imetimiza mika 46!!! kweli tunahitaji mabadiliko.

Nb:Imeandikwa na Fredy Kapara,mwanafunzi wa J.S.S Law mwaka wa 3
Nappy Girl said...

Tukumbushane maana ya uongozi..wat i knw uongozi si maneno(propaganda) bali uongozi ni vitendo.ningeomba TASAM ingefocus kwny kudumisha umoja wa watanzania mysore na kuavoid maneno matupu ya hewani bila vitendo....

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania