CURRENT NEWS

Sunday, November 15, 2015

MAKAMU WA RAIS AWAPA MOYO WACHEZAJI WA TAIFA STARS KUELEKEA MCHEZO WA MARUDIANO



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza Nahodha wa Timu ya Taifa Stars, Nadir Haroub 'Canavaro', baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta. 
Akizungumza na wachezaji hao baada ya mchezo huo, Mhe. Samia,aliwataka wachezaji na viongozi wa Stars kutovunjika moyo kutokana na matokeo ya mchezo huo, na kuwataka kuongeza juhudi na kujituma zaidi katika mchezo wa marudiano ili ukweza kupata matokeo mazuri zaidi.
''Japo mmefungwa lakini tumewaona jinsi mlivyojituma, msivunjike moyo na matokeo ya mchezo, kwani tumeowana mlivyocheza kwa kujituma, hivyo naamini hata ugenini mtaweza kupata matokeo mazuri zaidi mkiwa na moyo huo huo wa utaifa, juhudi na kujituma,
Mtangulizeni mungu kwa kila jambo na kwa uwezo wake naamini mtaenda kufanya vizuri katika mchezo wa marudiano, na nawatakieni safari njema leo usiku kuelekea mchezo huo wa marudiano, sisi wazee wenu na Watanzania wote tupo nyuma yenu tunawaombe muweze kuwatoa waarabu hawa wenye fitina kali katika mchezo wa Soka''. alisema Mhe. Samia 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Thomas Ulimwengu, baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.  Kulia ni Mbwana Samatta, akibugujikwa na machozi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta, baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Baada ya mchezo huo Samatta, alionekana kubugujikwa na machozi muda wote. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.  Picha na www.sufianimafoto.com
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishangilia sambamba na baadhi ya Viongozi bao la kwanza la Taifa Stars lililofungwa na Elias Maguli, katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia dhidi ya Algeria uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamal Malinzi, wakati walipokuwa Uwanja wa Taifa katika mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria  uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.
 Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
 Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria mtanange huo jana
 Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
 Ila moja kati ya kituko ilikuwa ni hiki kiti kilichokatika mguu mmoja eti katika mchezo wa kimataifa kama huu hwakupata kiti chenye hadhi kulingana na mchezo wenyewe
 Timu zikiwa tayari kuanza mtanange huo, hapa zikipigwa nyimbo za taifa
 Mudathir Yahya, akiwachora nane waarabu....
 Mbwana Samatta, akitesa Waarabu kwa vyenga,akiwageuza atakavyo..
 Waarabu waliimarisha ulinzi zaidi kwa Mbwana Samatta.....
Beki wa Stars, Shomari Kapombe, akiruka kwanja la mchezaji wa Algeria.....
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania