CURRENT NEWS

Tuesday, June 21, 2016

BEMBA AHUKUMIWA MIAKA 18 JELA

 Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Jean-Pierre Bemba, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kufuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ICC, kutokana na uhalifu wa kivita na unyanyasaji wa kingono.
Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi kwa makoso ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003.
Analaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu. Mawakili wa Bemba tayari wamesema kuwa watakataa faa kupinga hukumu hiyo.
Akitoa hukumu hiyo jaji Sylvia Steiner, alisema kuwa Bemba alishindwa kudhibiti waasi wake ambao walitumwa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Bemba alikuwa ametuma zaidi ya wapiganaji 1,000 kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumsaidia rais wa zamani Ange Felix Patasse, kukubiliana na jaribio la mapinduzi.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania