CURRENT NEWS

Saturday, June 4, 2016

HAKI ZA MTOTO TUNAPOELEKEA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA 16 Juni 2016

Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kimataifa kote duniani kwa lengo la kutambua thamani, utu , na umuhimu wa mtoto duniani. Mwaka 1990, uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ulipitisha Azimio la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto kilichopo Afrika Kusini waliouawa kinyama na iliyokuwa Serikali ya Makaburu ya nchi hiyo tarehe 16 Juni, 1976. 

Watoto hao walikuwa wakidai haki ya kutobaguliwa na haki nyingine za kibinadamu. Kwa kutambua umuhimu wa mtoto, Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kitaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kwa kutumia njia mbalimbali ikewemo vyombo vya habari (magazeti, redio runinga). 

Pia itaendesha kampeni katika mitandao ya kijamii (Intagram na facebook) iliyopewa jina la “#NAMPENDANITAMLINDA” ambayo itatoa fursa kwa watu mbalimbali Tanzania kupiga picha wakiwa na watoto na kuzituma “kupost” kwenye mitandao yao ya kijamii (Instagram na Facebook) na kisha kuandika (hush tag) “#NAMPENDANTAMLINDA”.

Lengo la kampeni ili kuimarisha juhudi za wadau mbalimbali katika kulinda na kuendeleza haki na maslahi ya watoto nchini. Kampeni hii itaanza Juni 1 na kuhitimisha kilele tarehe 16 Juni ambayo ni siku ya Mtoto wa Africa.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika mwaka huu ni “Migogoro na machafuko Afrika: Tulinde haki za Watoto” 

TAMWA inawaomba wadau mbalimbali wakiwemo wazazi, waalimu, viongozi, wasanii na wanajamii kwa kuonyesha upendo kwa watoto kwa kuithibitishia jamii kwa kutumia mitandao ya kijamii kuwa wanawapenda na watalinda haki zao.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania