CURRENT NEWS

Monday, June 6, 2016

HILLARY ASHINDA JIMBO LA PUERTO RICO

Image copyrightGETTY
Image captionHillary ashinda eneo la Puerto Rico
Vyombo vya habari nchini Marekani, vinaripoti kuwa mgombea wa urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton ameshinda uteuzi wa chama hicho katika eneo la Puerto Rico.
Ushindi huo unaimarisha matumaini yake ya kunyakua uteuzi wa chama hicho, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi wa Novemba mwaka huu.
Matokeo ya awali yanaashiria kuwa Bi Clinton atashinda kwa asilimia 60% ya kura ikilinganisha na asilimia 35% za mpinzani wake Bernie Sanders.
Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionBi Clinton atashinda kwa asilimia 60% ya kura ikilinganisha na asilimia 35% za mpinzani wake Bernie Sanders.
Bi Clinton sasa anahitaji chini ya wajumbe 30tu ili kushinda uteuzi wa chama hicho.
Ushindi huo ni afueni kubwa kwa Bi Clinton huku wakipiga kura katika majimbo ya New Jersey na California wakiajianda kupiga kura siku ya Jumanne.
BBC.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania