CURRENT NEWS

Sunday, June 12, 2016

IBADA YA KUMKUMBUKA ALI YAJAWA NA MIHEMKO

Bill Clinton
Ibada ya ukumbusho iliojawa na mihemko ya aina yake kwa bondia Mohammed Ali imefanyika katika mji alikozaliwa wa Louisville, Kentucky.
Baadhi ya mabondia na muigizaji Will Smith waliohudhuria hafla hiyo.
Umati watu 14000 ulisikiliza kwa makini watu wa tabaka na dini tofauti wakimuomboleza mohammed ali kutokana na umahiri wake katika ulingo wa michezo na pia alivyoitunza jamii, huku wakisifu mchango wake katika kuimarisha amani duniani na haki za binadam.
Umati wa watu waliohudhuria hafla ya kumbukumbu hiyo
Mkewe Ali, Lonnie Ali, anasema mumewe alikabiliwa na masaibu si haba, bila kuonyesha hasira, na kuwataka watu kufuata mfano wake
Mkewe Muhammad Ali
Katika taarifa, rais wa Marekani Barrack Obama, alimtaja Ali kama mtu shupavu, aliyeng'aa na aliyekuwa na ushawishi mkubwa kuliko mtu yeyote wa kizazi chake.
Msafara wa mwili wa Muhammad Ali kabla ya kuzikwa nyumbani Louisvile Kentucky siku ya Ijumaa
Rais wa zamani Bill Clinton, alikumbuka utanashati, ucheshi na utu aliooonyesha marehemu Ali, wakati akikabiliana na machungu ya ugonjwa uliomdhoofisha.BBC
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania