CURRENT NEWS

Sunday, June 12, 2016

KARIBU WATU 50 WAUAWA ORLANDO MAREKANI


Watu 50 sasa wanajulikana kuuawa kwa kupigwa risasi wakati wa shambulizi lililotokea kwenye baa moja katika jimbo la Florida, na kuwa moja ya mashambulizi mabaya zaidi katika historia ya Marekani.
Watu wengine 50 wako hospitalini. Vyombo vya habari vimemtambua mwanamme ambaye alitekeleza shambulizi hilo katika mji wa Orlando kuwa raia wa Marekani, Omar Mateen.

Image copyrightCBS
Image captionOmar Mateen, aliyefyatua risasi Orlando

Mwanamme huyo wa umiri wa miaka 29, alikuwa amejihami kwa bunduki mbili wakati alifyatua risasi katika baa ya Pulse siku ya Jumaosi
Aliwashika mateka karibu watu 30 kabla ya polisi kumpiga risasi na kumuua.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania