CURRENT NEWS

Wednesday, June 8, 2016

LEAT YAWATAKA WANANCHI KUHIFADHI MAZINGIRA NA MALIASILINi Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Asumpta Mshama akihutubia wananchi wakati wa sherehe za siku ya mazingira duniani, katika kijiji cha Lugodalutali, wilaya ya Mufindi


 kikundi cha sanaa kutoka kijiji cha mapogoro kikihamasisha utunzaji wa mazingira na maliasili ktk sherehe za siku ya mazingira zilizo fanyika tarehe 3 June 2016 kijijini Lugodalutali. Kikundi hiki kinalelewa na Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT)

 LEAT yagawa vitabu na vipeperushi vinavyotoa elimu ya mazingira na maliasili


na fredy mgunda,iringa

Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) imewaasa wananchi kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa mazingira na maliasili na kuzitaka mamlaka za usimamizi wa mazingira na maliasili kutimiza wajibu wao kwakuwa serikali imewaamini na kuwapa jukumu hilo.

Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Mufindi katika maadhimisho ya siku ya mazingira iliyofanyika katika kijiji cha Lugoda Lutali wilayani Mufindi mkoani Iringa Afisa Mawasiliano wa LEAT Miriam Mshana ,alisema kuwa uharibifu wa mazingira umechangiwa kwa sehemu kubwa na shughuli za binadamu ikiwa ni pamoja na ukataji miti ovyo bila kupata vibali na uvunaji haramu wa wanyamapori, usio rafiki kiuchumi na kimazingira.

 Mshana alisema, uvunaji wa kasi hasa wa misitu umeathiri na kuchangia mabadiliko ya tabia nchi, kuiweka nchi katika hatari ya kuwa jangwa. Uvunaji haramu wa wanyamapori hususan tembo umeipa hasara taifa.
 ‘’’’Kwa mujibu wa ripoti ya Mtaalam Mashuhuri wa tafiti za tembo duniani, Ian Douglas Hamilton, kwa mara ya kwanza mwaka 1976 alifanya utafiti wa angani, Tanzania kwa ujumla ilikuwa na tembo 316,000, ambayo ilikuwa idadi kubwa sana ikilinganishwa na maeneo mengine duniani’’’’’alisema mshana 

Kwakufanya hivyo tutakuwa tunaitikia wito wa kaulimbiu ya mwaka 2016 ya siku ya mazingira duniani-‘Shiriki kufanya dunia mahali pazuri’. 

Jowika Ksunga ni mkuu wa wilaya ya Mufindi nae alisema, Mwaka 1976, mbuga ya Selou pamoja na maeneo jirani ilikuwa na idadi ya tembo109,000,Utafiti uliofanywa mwaka 2013, ulibaini kuwa mbuga ya Selou ilikuwa  na tembo 13,084 pekee.

Kasunga alisema takwimu hizo zinaashiria hatari ya kutoweka kabisa kwa tembo katika nchi yetu na itaathiri biashara ya utalii ambayo ilikuwa ikitoa mchango mkubwa katika pato la taifa.

‘’’’’’’Maeneo mengi ya mijini yamechafuliwa kwa utupaji taka ovyo, hivyo kuharibu mandhari ya miji yetu na kuchangia katika magonjwa ya milipuko ikiwemo kuhara na kipindupindu, alisema Kasuga.

Alisema, utupaji taka ngumu na zenye sumu karibu na makazi ya watu au vyanzo vya maji, umeleta athari kubwa kiafya kwakuwa kemikali hizo hupenya ardhini na kudhuru ardhi na vyanzo vya maji, hasa kwa wananchi wanoishi karibu na viwanda na sehemu za uchimbaji madini.

 “Inasikitisha kuwa wamiliki wa viwanda vingi na machimbo ya madini wanakiuka sheria ya mazingira lakini pia wameshindwa kuwajibika kwa jamii zinazo wazunguka ambazo ndio wadau wakubwa wa biashara zao, kwa kaidi kuchukua hatua za kuzuia uharibifu wa mazingira hata baada ya athari kutokea”, alisema Jowika’’’’’’’’’

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Asumpta Mshama alisema kuwa shirika la LEAT limekuwa mstari wa mbele kwa zaidi ya miaka 20, katika kusimamia mazingira nchini katika sekta ya madini, viwanda, machinjio na mazingira kwa ujumla.

Asumpta alisema taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa mwezi Aprili, 2016 inaonesha takribani watu milioni 2 hufa kila mwaka duniani na zaidi ya watu bilioni moja hupatwa na magonjwa yanayo sababishwa na uchafuzi wa mazingira


‘’’’’Iwapo serikali, wananchi na wamiliki wa viwanda na machimbo ya madini, kila mmoja akitimiza wajibu wa kutunza mazingira tutakuwa natekeleza haki ya kuishi, haki ya afya bora na ustawi, kama ambavyo serikali ilivyo ridhia katika mikataba mbalimbali ya kimataifa ikiwemo mkataba wa Stockholm nchini Sweden  na Rio De janeiro nchini Brazil’’’’’’’’alisema Asumpta
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania