CURRENT NEWS

Monday, June 6, 2016

MBUNGE MWIGULU NCHEMBA APOKELEWA KWA SHANGWE JIMBONI KWAKE IRAMBA

Waziri  wa  Kilimo ,Mifugo na  uvuvi Bw  Mwigulu Nchemba  akifurahia  zawadi ya maboga  aliyepewa na  wananchi wa  kijiji  cha KilaMpanda  jimbo la Iramba mkoa  wa  Singida wakati wa ziara  yake ya  kuwashukuru  wananchi wa  jimbo  hilo kumchagua bila kufanya kampeni mwaka jana kuendelea  kuwa mbunge wao kwa  kipindi  cha pili sasa
Wananchi  wa jimbo la Iramba kata ya Kilampanda  wakimpokea  mbunge  wao Bw Mwigulu Nchemba kwa  zawadi za maboga wakati wa ziara  yake  jimboni  humu jana Juni 5
Mbunge wa  jimbo la Iramba ambae ni waziri wa  kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  akikabidhiwa  zawadi ya boga na  wananchi wa  kijiji  cha Kilampanda  wilaya ya Iramba mkoa wa Singida  wakati wa  ziara  yake  jimboni  humo Juni 5 kwa ajili ya kuwashukuru na kutekeleza ahadi  zake 
Mbunge Nchemba  akiteta jambo na katibu  wake Bw Daud  Ntukuna  kushoto
Wananchi wa kata ya Kilampanda  wakimpokea mbunge  wao Bw Nchemba kwa matawi ya miti
Mwigulu Nchemba  akipokelewa kwa  shangwe  jimboni kwake Iramba
Mbunge Nchemba  akiwapungia mikono wananchi  wake  baada ya  kupokelewa  wakati wa ziara ya  kuwashukuru kwa kumchagua
Mmoja kati ya  wananchi  akimshukuru mbunge Nchemba kushoto kwa utekelezaji wa ahadi zake  jimboni
Mbunge Nchemba  akimpa mpiga kura  wake namba yake  ya simu
Mbunge Nchemba  akiwasili kijiji  cha Kilampanda kwa ziara

mwananchi  wa  kata  ya  kilampanda  akimkumbatia  mbunge Nchemba  kwa  furaha
Mbunge wa Iramba na  waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi  akipokelewa jimboni kwake
katibu  wa CCM Iramba akimkaribisha  mbunge Mwigulu
Mbunge wa  jimbo la Iramba na waziri wa  kilimo ,Mifugo na Uvuvi  akikabidhi ahadi  yake ya  bati kwa wananchi wa kijiji cha Kilampanda kwa ajili ya ujenzi wa kituo  cha afaya  hadi  sasa amegawa bati 1800 zenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni  45  kama  sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa  wananchi hao kwa  lengo la ujenzi wa Zahanati ,mabweni , vyumba vya madarasa na nyumba za  walimu na waganga ,nondo 450  zenye  thamani ya zaidi  tsh milioni 7.6
Waziri  wa  Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  akifurahia  zawadi ya mbuzi aliyopewa na  wananchi  wake wakati wa ziara ya kuwashukuru kwa kumchagua katika  uchaguzi mkuu mwaka jana  pasipo  kufika kufanya kampeni ,Mwigulu amekuwa akitumia siku za mapumziko  bungeni kuzunguka jimboni mwake  kufanya mikutano ya kushukuru  wananchi  kila Jumamosi na jumapili
Mbunge Mwigulu akitembea kwa  miguu na  wananchi wake katika moja kata ya bonde ambalo ni  hesemu ya barabara inayolalamikiwa na uwananchi kutokana na ubovu eneo  hilo halina daraja
gari la waziri likipita  eneo korofi la barabara
waziri Nchemba  akiwa na  wapiga kura  wake
Lori  lililobeba bati  ambalo  husambaza  ahadi za mbunge Mwigulu jimboni
Mbunge Mwigulu  akisalimiana na  wapiga kura  wake
Mbunge  wa  jimbo la Iramba Bw Mwigulu Nchemba  akiongea na  vijana  kwa ajili ya  kuwasaidia  vifaa vya michezo wakati wa ziara  yake jimboni  humo jana  juni 5 PICHA NA MATUKIODIMABLOG
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania