CURRENT NEWS

Saturday, June 4, 2016

MECHI YA TAIFA STARS NA MISRI YAWAKUTANISHA WADAU WA MICHEZO TAIFA

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa soka nchini, kulia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanznaia (TFF), Jamal Malinzi, Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini FAT Said El Maamry, upande wa kushoto ni Mwenyekiti wa zamani wa TFF Muhidini Ndolanga na  Rais wa zamani wa TFF Ndugu Leodgar Tenga muda mfupi kabla ya kuanza ka mechi ya Taifa Stars na Misri.
 
 Viongozi na wapenzi wa soka wakiimba kwa pamoja wimbo wa Taifa kabala ya mechi kuanza.
 Viongozi na wadau wa michezo wakitoa heshima kwa kusimama wakati wa wimbo wa Taifa.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze akizungumza na Khamis Mgeja kabla ya mechi haijaanza.
 Timu ya Taifa Stars ikipeleka mashambulizi kwenye goli la timu ya Misri hata hivyo mpaka mchezo umeisha Misri waliibuka na ushindi wa 2-0.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akitazama mechi ya Taifa Stars, wengine pichani ni Rais wa TFF Ndugu Jamal Malinzi na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Frederick Sumaye.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania