CURRENT NEWS

Wednesday, June 22, 2016

MJI WA GARABOULLI LIBYA WACHAFUKA

Maofisa wa serikali nchini Libya wanaarifu kwamba watu ishirini na watano wameuawa na maelfu wengine wakijeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye duka la kuhifadhia risasi upande wa magharibi ya mji wa Garaboulli.
Duka hilo la kuhifadhia silaha linaarifiwa kuwa lilikuwa likitumiwa na jeshi la nchi hiyo lililoko katika mji wa Misrata, mji ulioko karibu na pwani.
Inaarifiwa chanzo cha vifo vya watu hao ishirini na watano ni ugomvi uliozusha mapigano baina yao na wakaazi wa mji wa Garaboulli.
Mlipuko huo ulitukia mara tu baada ya wenyeji wa mji huo walipoingia katika duka hilo lililotelekezwa. Na mpaka sasa bado chanzo cha mlipuko huo hakijafahamika.
Mzalishaji vipindi wa BBC aliyekuwa karibu na eneo la tukio ameeleza kwamba barabra ya pwani mwa Garaboulli imefungwa na kwamba anasikia sauti za milio ya risasi kwa mbaali.
mchanganyiko wa raia wenye silaha na wanamgambo kutoka mji wa pwani wanaendesha upekuzi kwenye vituo vya ukaguzi kando kando ya barabara ya pwani, na magari yanayojaribu kupita eneo hilo yanafanyiwa upekuzi mkali ingawa haijajulikana wanapekuliwa kwa suala gani.
Hali katika eneo hilo inaelezwa kuwa ya hatari.wakaazi wa mji wa Gharabouli, amabao wamezungumza na BBC kwa njia ya simu,wamesema kwamba tukio hilo limesababishwa na askari kutoka katika kikosi cha jeshi kilichoko mji wa Misuratan walipotaka kununua bidhaa kisha wakakataa kulipia bidhaa hizo.
Katika sakata hilo inasemekana mmiliki na muuzaji wa duka hilo alipigwa risasi na kufariki dunia na baadaye kuliripotiwa mapigano ya kulipiza kisasi kati ya wanamgambo na wakaazi wa eneo hilo .
Duka hilo lililokuwa chanzo cha tatizo lilichomwa moto baadaye na nyumba ya familia ya mmiliki wa duka hilo iliyokuwa jirani,na baada ya tukio hilo wakazi wengine wenye silaha walipinga mashambulizi hayo na uwepo wa jumla wa wanamgambo kwamba na wakati huo huo duka la jirani lenye kuuza silaha pia lilikuwa na malori yenye mzigo wa biashara hasa vilipuzi liliripuka.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania