CURRENT NEWS

Saturday, June 4, 2016

MKUTANO WA POLISI NI FURSA YA KUIMARISHA ULINZI WA AMANI-TANZANIA


Naibu Kamishna wa polisi na Mkuu wa operesheni maalum za polisi, Daniel Nyambabe.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J.Msami)

Mkutano wa aina yake wa wakuu wa polisi kutoka nchi 109 wanachama wa Umoja wa Mataifa unaendelea mjini New York, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ameshuhudia kile alichokiita polisi werevu wakileta tofauti katika utawala wa sheria na kuandaa mazingira ya amani na maendeleo.

Katika ujumbe wake kwa maandishi Katibu Mkuu amesisitiza kuwa polisi ni muhimu kwani wanalinda jamii, huleta utulivu na kujiamini.

Kwa upande wake Tanzania inayowakilishwa katika mkutano huo imesema utasongesha juhudi za ulinzi wa amani hususani katika nchi za maziwa makuu.


Katika mahojiano maalum na idhaa ya Radio ya Umoja wa Mataifa mwakilishi wa Tanzania katika mkutano huo, Naibu Kamishna wa polisi na Mkuu wa operesheni maalum za polisi, Daniel Nyambabe amesema kwakuwa nchi nyingi bado zinahitaji ulinzi wa amani barani Afrika hii ni fursa ya kuuboresha kwani.
UN.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania