CURRENT NEWS

Wednesday, June 1, 2016

RAIS WA WACHIMBA MADINI AJITOSA KUMSAIDIA RAIS DR MAGUFULI

 Rais  wa  shirikisho la  wachimbaji madini Tanzania (FEMATA ) Bw  John Bina  akitambulishwa  mbele ya  balozi wa China nchini (hayupo pichani) kulia ni waziri wa Kilimo ,Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba
 Bw  John Bina  akihamasisha uchangiaji wa madawati  mashuleni


  balozi  wa Chini Nchini Tanzania Dr Lu  Yonq.ng  katikati  akiwa na viongozi wa mkoa wa Shingida  kutoka  kulia mkuu wa  mkoa wa Singida Bw Methew Mtigumwe,waziri wa  kilimo ,Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ,mbunge wa  viti maalum mkoa wa Singida Bi Martha Mlata  na Rais wa FEMATA Bw John Bina

Na MatukiodaimaBlog ,

RAIS wa shirikisho la vyama vya   wachimbaji    madini Tanzania (FEMATA) ametoa wito kwa wachimbaji wote  yakiwemo makampuni makubwa ya uchimbaji   wa madini  kujitokeza kumuunga mkono  Rais Dr John Magufuli   katika harambee ya kuchangia madawati kwa shule mbali mbali hapa nchini.

Huku akisifu  mwitikio mzuri  wa kampuni ya Sunshine Minning  kwa  kuunga kuitikia wito  huo kwa  kuchangia madawati 100 yenye thamani ya Tsh milioni 85,000 kwa Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida  .

Akizungumza na  waandishi wa  habari jana ,Rais  wa FEMATA  John Bina alisema  kuwa Shirikisho  lake  limelazimika  kumsaidia Rais Dr Magufuli kuhamasisha uchangiaji wa madawati  kwa  wanachama  wake ili kumaliza kabisa tatizo  hilo la uhaba  wa madawati  na  kuona   sekta ya  elimu nchini  inaboresheka  zaidi  kwa   kuhakikisha  wanafunzi  hawakai chini.

Bw Bina  alisema  kuwa katika   kuunga mkono  jitihada za  serikali wao kama sehemu ya  wadau wa maendeleo katika Taifa hawakupenda  kuwa  nyuma kujitokeza  kuchangia madawati hasa  ukizingatia  kuwa elimu  bora  ni mwanzo wa  kuwa na taifa  bora .

"Suala   hili la elimu si la  serikali pekee kila mmoja kwa nafasi yake ana umuhimu katika  kuboresha  elimu  nchini  na si  vema  kwa  kila  jambo  kuitazama  serikali ......serikali  ina  nafasi yake  ila  na sisi  wadau  tuna nafasi  yetu katika  kuiunga mkono serikali pia  wanafunzi  wananafasi yao .... walimu na  wazazi  pia " alisema rais Bina

Hata   hivyo  aliwataka   wadau  wengine  na  wananchi  mmoja  mmoja kwa nafasi yake  kujitokeza kuunga mkono uchangiaji wa madawati  ili  kumaliza kabisa kero  hiyo ya  uhaba wa madawati  mashuleni.

Alisema  wao kama wadau  wa maendeleo  kupitia FEMATA wataendelea  kuunga mkono  jitihada  mbali mbali  zinazoendelea  kufanywa na serikali ya Rais Dr Magufuli  jitihada  zenye  lengo la  kulifanya Taifa   kuzidi  kuwa mbele  kimaendeleo.

Pia  alisema  kwa wadau  wa  sekta   hiyo ya madini  pekee  kama  kila mmoja atajitolea  kuchangia madawati  upo  uwezekano mkubwa wa  zoezi   hilo kukamilika mapema   zaidi na kuwataka  wadau  wengine   mbali ya wale wa madini  nao kwa nafasi  zao  kujitolea madawati  badala ya  kuiachia  serikali pekee.

“ Ninakusudia  kama  Rais  wa FEMATA  kuwakutanisha  wachimbaji  wote mbali na mambo mengine  tutaangalia  ushiriki  wetu katika masuala  ya kijamii yakiwemo ya uchangiaji wa madawati”

Hata   hivyo mkuu  wa  mkoa  wa  Singida Bw Methew Mtigumwe mbali ya  kupongeza harakati  za Rais  huyo wa FEMATA  kwa  kuunga mkono agizo la rais kwa  kujitolea  kuhamasisha uchangiaji wa madawati  bado  alisema  kuwa jambo  hilo ni  jema na linapaswa  kupongezwa zaidi.

Alisema katika mkoa  wa Singida  kila mkuu wa  wilaya ameagizwa  kusimamia utekelezaji wa agizo la Rais la upungufu wa madawati katika eneo lake na  kuwa mkoa umejipanga  kumaliza kabisa  kero  hiyo ya uhaba wa madawati .
MWISHO
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania