CURRENT NEWS

Tuesday, June 7, 2016

SHOW YA KANYE WEST YAKUMBWA GHASIA NEW YORK

 
Shoo ya ghafla iliyofanywa na mwanamuziki raia wa Marekani Kanye West mjini New York, ilifutwa baada ya maelfu ya mashabiki kufika eneo la shoo na kuzua fujo.
Zaidi ya mashabiki 4000 walifika katika ukumbi wa Webster ulio na uwezo wa kuchukua watu 1500.
Mashabiki walimiminika barabarani na kisha kupanda juu ya magari wakichungulia kupitia madirisha, angalu kumuona mwanamuziki huyo.
Kanye alisema kuwa atafanya shoo hiyo ya ghafla kwenye mitandao ya kijamii baada ile ya mji wa New York kufutwa kutokana na hali mbaya ya hewa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania