CURRENT NEWS

Friday, June 3, 2016

VIDEO YAWATIA MASHAKANI WANAFUNZI WALIOFANYA MTIHANI INDIA

Wanafunzi 14 walioongoza katika matokeo ya mtihani wa mwisho katika jimbo la Bihar nchini India watalazimika kufanya tena mtihani kufuatia madai kwamba walihusika na udanganyifu, serikali ya jimbo hilo imsema.
Uamuzi huo uliafikiwa baada ya mmoja ya wanafunzi hao Ruby Rai mwenye umri wa miaka 17 kuviambia vyombo vya habari kwamba sayansi ya siasa inahusisha kupika.
Kanda ya Video ya mahojiano hayo na yale ya wengine ilisambazwa sana. Mwaka uliopita, wazazi wa wanafunzi katika jimbo hilo walipigwa picha wakipanda kuta za shule ili kutoa majibu kwa wanafunzi wanaokalia mtihani.
Serikali ya jimbo hilo ilikuwa imetangaza hatua kali kama vile faini na vifungo jela kwa lengo la kuangamiza uovu huo mwaka uliopita.
Alama za chini zilizopatikana katika matokeo yaliotangazwa wiki iliopita zilichukuliwa kama ishara kwamba hatua zilizochukuliwa zimefanikiwa.
Image copyrightBIHARPICTURES.COM
Image captionWanafunzi wanaokalia mtihani
Hiyo ni hadi kanda ya video ya Ruby Rai ilivyopeperushwa hewani.
Serikali imesema kuwa matokeo yake na yale ya Saurabh Shrestha ambaye alikuwa wa kwanza katika somo la sayansi na alishindwa kujibu swali rahisi la somo la kemia yamepigwa marufuku mara moja
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania