CURRENT NEWS

Wednesday, June 1, 2016

WAZIRI NCHEMBA AAGIZA MAOFISA USHIRIKI SINGIDA KUCHUKULIWA HATUA
Waziri  wa  kilimo ,mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali  kuingia  ukumbi wa mkutano kati yake na wakulima wa Tumbaku Manyoni
Mbunge Mwigulu Nchemba wakati akisaini kitabu cha  wageni  ofisi ya mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida
Waziri Nchemba  akiingia ukumbi wa mkutano kati yake na  wakulima wa Tumbaku manyoni
Wakulima wa Tumbaku  wakisalimiana na waziri Nchemba 
Baadhi ya madiwani  wakulima wa Tumbaku manyoni wakimpokea  waziri Mwigulu Nchemba
Baadhi ya  wakulima wa Tumbaku  wakiwa  ukumbi wa mkutano kati yao na waziri Nchemba

Waziri wa  Kilimo , Mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  akizungumza na  wakulima wa Tumbaku wilaya ya manyoni mkoa wa Singida jana
Diwani  wa kata ya Mitundu wilaya ya Manyoni Bw Andrea Madole  akimkabidhi nyalaka mbali mbali za uthibitisho wa michango kandamizi  wanayobambikizwa  wakulima wa Tumbaku na Kitengo  cha AMIS   waziri wa  kilimo ,mifugo na Uvuvi Bw Mwigulu Nchemba ambae alitangaza   kufuta michango  hiyo
Wakulima wa Tumbaku  wakitoa kero  zao kwa  waziri Nchemba (hayupo pichani)
Wabunge  wakisikiliza kero  za  wakulima wa Tumbaku
waziri wa Mifugo na uvuvi Bw Mwigulu Nchemba  (kushoto) akimsikiliza kwa makini kilio  cha wakulima wa Tumbaku  wilaya ya Manyoni wakati wa  mkutano wa  waziri Nchemba na wakulima wa Tumbaku  uliofanyika  ukumbi wa CCM Manyoni jana
..................................................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog,Manyoni

WAZIRI wa  kilimo ,mifugo na  uvuvi  Bw Mwigulu  Nchemba amefuta michango  hewa iliyokuwa ikichangiwa na wakulima wa Tumbaku  kwa  UNION kwa  kupitia  kitengo  cha AMIS huku akiagiza serikali  ya  wilaya ya Manyoni  kuwachukulia hatua  kali aofisa  ushirika mkoa  Andru Msafiri na afisa  ushirika Wilaya   hiyo Bw Alfred Sekiete iwapo watabainika  kuhusika  deni la bilioni  7  ambalo wanadaiwa benki wakulima  wa tumbaku.

Waziri Nchemba  alilazimika kutoa maagizo  hayo  baada  ya  wakulima  wa zao hilo la Tumbaku  kulalamikia utaratibu mbaya wa baadhi ya  viongozi wa UNION na APEX pamoja na baadhi ya maofisa  ushirika   kujinufaisha  kupitia mgongo  wa  wakulima hao.

Akitoa agizo  hilo  jana mjini Manyoni  wakati wa  mkutano  wa  pamoja kati yake na  wakulima wa  Tumbaku na viongozi  mbali mbali  wa Serikali  ya  wilaya ya Manyoni na wabunge  wanaotoka  wilaya ya Maeneo  yanayolimwa Tumbaku  mkoani Singida.

Waziri Nchemba  alisema  kuwa  baadhi  ya mambo  ambayo serikali  ya Rais Dr John Magufuli  haipendi  kuona ni  pamoja na  wakulima kubebeshwa mizigo mikubwa ambayo kimsingi haiwasaidii kupiga hatua kimaendeleo  zaidi ya  kuwatesa .

Alisema  inashangaza  kuona   wakulima  hao  kuendelea  kuumizwa na  viongozi  wachache ambao  wamegeuza  wakulima ni  kichaka cha  wao  kujificha  kujinufaisha  kupitia wakulima.

“ Mambo  ya ajabu  sana  hiki kitu  kinaitwa AMIS ni kuwatoza  wakulima michango ya ajabu ajabu  eti  wakulima  kutozwa  dola 1200 kwa  ajili  ya kusafirisha Tumbaku toka  Dar es Salaam kwenda UNION   pia  wanachangia dola 10 kwa  kutunza  kumbukumbu zao  ,dola 3 kupakia na  kushusha mara mchango kwa ajili ya ADMIN   mambo ya ajabu kabisa wakulima wanahusika  vipi na malipo maadmin yani wanatumia lugha  za  kijanja kijanja  kuwaibia  wakulima ADMIN wa makundi kama yale ya Whatsap kwa wakulima  tena…sasa kuanzia leo natangaza  kufuta michango  hii isiyo na maelezo ya kutosha na kuagiza  kujipanga upya kwa  kuwashirikisha   wakulima na taarifa  hiyo ndani ya siku 7 niipate “

Waziri chemba  alisema  kuwa kabla ya  kuanza  kuwatoza  wakulima hao michango ni  vizuri  makubaliano ya  michango  hiyo yafanyike  upya kwa kuwashirikisha  wakulima na sio kuendelea  kutumia taratibu  za  zamani ambazo ni mzigo kwa  mkulima.

Kuhusu maafisa  ushiriki  kudaiwa  kukopa  benki  kupitia mgongo wa  wakulima  wa  tumbaku na  kupelekea  wakulima hao  kudaiwa  deni  benki  la Tsh bilioni 7 aliagiza mkuu wa  wilaya ya Manyoni kuagiza wakaguzi  na wataalam wake  kufanya  uchunguzi  na iwapo itabainika  kuwa maofisa  hao  walihusika na deni  hilo  hatua  stahiki  kuchukuliwa dhidi 

Alisema  ni  kosa  kwa maofisa  ushirika   kukopa  kwa  udhamini  wa  wakulima   wakati  wao si  wazalishaji wa mazao hayo ya  kilimo na kuwa maeneo  mengi wakulima  walikuwa wakiwalipia madeni benki maofisa   hao ambao huomba  mikopo kupitia vyama  vya msingi vya  wakulima na wakati mwingine hushirikiana na benki kutoa mkopo mkubwa ili  nao waweze kugawana .

Pia aliagiza  UNION  kufanya kazi ya  kuwasaidia   wakulima na sio  kuwakandamiza   wakulima na  kuwa maeneo  mengi nchini ambayo  UNION wapo kumekuwa na migogoro na kero nyingi kwa  wakulima na kuwa mazao ambayo wakulima hawana UNION kama Mahindi , mpunga na alizeti wakulima wanafanya  shughuli  zao pasipo migogoro  hivyo kuzitaka UNION zinazojihusisha na  wakulima wa Tumbaku , Korosho ,pamba na mazao mengine  kujitathimini  vinginevyo hazina maana kuwepo.

Aidha  waziri Nchemba  aliagiza benki ya CRDB kuwalipa pesa  zao  zote wakulima  wa Tumbaku ambao wamemaliza madeni yao ya  pembejeo  na kuendelea  kuwadai wanaodaiwa na si vinginevyo .

Mbunge  wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu  alisema  kuwa  kilio  kikubwa  cha   wakulima wa Tumbaku Manyoni ni uwepo  wa mtu kati katika kilimo  hicho hivyo  kuwatesa  wakulima hao na  kuwa  UNION  na APEX  bado si ukombozi kwa  wakulima wa  zao la Tumbaku kwani  alisema  wakulima wamekuwa wakilipwa asilimia 50 ya mauzo ya mazao yao na benki ya CRDB  na asilimia 50 nyingine  kushikiliwa na benki kwa mkopo wa vyama  vyao  vya msingi hata kama mkulima  husika hadaiwi.

Mwenyekiti wa  muungano  wa  vyama  vya msingi  vya wakulima  wa Tumbaku (AMCOS) Bw Khalifa Huruma akitoa  taarifa ya  muungano huo alisema  kuwa maofisa  ushirika  wawili wa wilaya na mkoa kila mmoja amekopa dola 2000 wakati  wao si wakulima wa  tumbaku .
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania