CURRENT NEWS

Sunday, July 31, 2016

DC MSHAMA ATAKA WAFANYABIASHARA SOKO LA MLANDIZI WATAKIWA KULIPA USHURU

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Assumpter Mshama akizungumza na wawakilishi wa wananchi waishionamtaa wa Kidimu Kibaha mjini mkoani hapa walipofika kuwawakilisha wenzao wanaodai ardhi yao kuchukuluwa pasipokulipwa fidia. NA MPIGA PUCHA WETU.

Na Omary Said, Mlandizi
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama amewataka wafanyabiashara katika soko la Mlandizi lililopo Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani kulipa ushuru ili kuiwezesha halmashauri hiyo kuimarisha miundo mbinu.

Mshama aliyasema hayo alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa wafanyabiashara wa sokoni mbapo amewaambia wafanyabiashara hao kulipa ushuru wa shilingi mia mbili na kuachana na desturi ya kulipa shilingi 100 bila kupewa risiti kitu ambacho kinawakosesha mapato wao wenyewe ambayo yangetumika kuboreshea miundombinu ya soko hilo.

Aidha amewahakikishia wafanyabiashara hao kuwa atshirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Tatu Selemani katika kuhakikisha miundombinu ya soko hilo inaimarishwa ili waweze kuvuna walichokipanda kwani hauwezi kuvuna bila kupanda.

"Niwahakikishie kwamba hii serikali ya awamu ya Tanoinayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ipo imaraMkuhakikisha inawawatumikia ipasavyo wananchi hususani wanaoitwa wanyonge kwa maana ya wenye kipato cha chini," alisema Mshama.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Pwani Aly Ndauka aliabza kwa kumpongeza Mkuu huyo kwa kuleta matumaini mapya katika kuleta maendeleo ya wilayani humo na hiyo inatokana na namna anavyofanyakazi ya kupwenda kwa wafanyabiashara na kuzungumza nao ili kubaini changamoto zinazowakabili.

"Katika kipindi kifupi unaonekana ni kiongozi unayejali wananchi unawaongoza kwani kipindi kifupi umekuwa na mikutano na wafanyabiashara ambao ndio wanaoziwezesha halashauri kukusanya mapato haswa ukizingatia,"


Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri Tatu aliwataka wafanyabiashara hao kuendeleza umoja katika shughuli zao pamoja na kumpatia ushirikiano Mkuu huyo ili kwa pamoja waweze kulisukuma gurudumu la maendeleo la wilaya hiyo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania