CURRENT NEWS

Sunday, July 31, 2016

LIL WAYNE ATOA MSUKUMO KWA HOTUBA YA CLINTON

Mashabiki wa mwanamuziki wa Marekani Lil Wayne wamekuwa wakidai kwamba huenda maneno ya wimbo wa msanii huyo yalitoa msukumo kwa hotuba ya bi Hillary Clinton.
"When there are no ceilings, the sky's the limit," {Iwapo hakuna paa la nyumba basi ,kikomo ni mbingu},Clinton aliliambia kongamano la chama cha Democrat.
Alikuwa akizungumza baada ya kukubali tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Democrat.
Mashabiki wa msanii huyo wa muziki wa rap sasa wamezua uvumi katika mtandao wa Twitter wakipendekeza kuwa huenda ameshinikizwa na wimbo huo unaosema kuwa iwapo hakuna paa kikomo ni mbingu.
Hakujakuwa na tamko lolote kutoka kwa Hillary Clinton ama timu yake lakini Lil Wayne amekuwa akihusisishwa.
Amewaambia maripota kwamba yeye hana tatizo lakini akakiri kwamba hajaiona hotuba hiyo.
Baadaye alichapisha ujumbe wa kumuunga mkono mgombea huyo wa urais.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania