CURRENT NEWS

Wednesday, July 20, 2016

WANAWAKE WAISLAM 10,000 WACHOSHWA KWA UPWEKE NIGERIA

Zaidi ya wanawake waislamu 10,000 wameomba watafutiwe waume watakaowaoa.
Wanawake hao wameomba shirika moja la kiislamu Hizba linahudumu katika eneo la Kano lililoko kaskazini mwa Nigeria kuwaunganisha na kugharamia ndoa ya halaiki.
Kamati maalum ya Hizba ndiyo iliyopewa jukumu hilo la kuwaondolea upweke maelfu ya wanawake waislamu.
Madhumuni ya kamati hiyo ya Hizba ni kupunguza idadi ya wanawake waislamu ambao hawajaolewa.
Hizba huwakutanisha wanawake na wanaume waislamu kwa lengo la kuwaoza kama watakubaliana kwa misingi ya dini ya kiislamu.
Wanawake wengi walimueleza muandishi wetu mjini Kano kuwa wamekuwa wakitafuta waume wazuri wa kuwaoa lakini hawajabahatika.
Image captionHakuna tarehe maalum iliyotengwa
Upweke ukawalazimu kuomba msaada kutoka kwa shirika hilo la Kiislamu.
Wengine wanasema kuwa hawajakuwa na uwezo wa kuandaa sherehe ya nikaa au ndoa katika dini ya kiislamu kwa hivyo wanasubiri ndoa hiyo ya halaiki kupunguza gharama.
Hakuna tarehe maalum iliyotengwa
Takriban wanandoa 5,000 wamefunga pingu za maisha tangu mradi huo uanzishwe mwka wa 2012
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania