CURRENT NEWS

Thursday, July 28, 2016

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NCHI MH:MWIGULU NCHEMBA ATUA MGODI WA NYAMHUNA UNAODAIWA KUTESA NA KUUA MTANZANIA MMOJA,AWAKAMATA WAHUSIKA(WACHINA NA WATANZANIA) WANAOSADIKIKA KUHUSIKA.

 waliokamatwa wakiwa chini ya ulinzi.

 kijana akoinyesha majeraha aliyopata kutokana na mateso.


picha kijana huyu akiteswa na mchina huyo.


Waziri wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu Nchemba hii leo amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyofanywa na raia wa china wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro-Geita dhidi ya wafanyakazi/vibarua ambao ni watanzania.

Takribani wiki moja sasa kumekuwa hali ya sintofahamu dhidi ya picha zinazoenezwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari zikionesha raia wa tanzania anayefanya kazi kwenye mgodi tajwa akiteswa na kufanyiwa vitendo vya kinyama na mwajili wake ambaye ni raia wa china.
Imemlazimu waziri mwenye dhamana na usalama wa raia na mali zao kupitia wizara ya mambo ya ndani kufika eneo la mgodi kujiridhisha kwa taarifa zilizotapakaa na kubeba simanzi kwa watanzania.

Mwigulu Nchemba amejiridhisha kuwa kulikuwepo na tukio hilo la mtanzania kuteswa na huyo mwajili wake kipigo kilichopelekea kupoteza fahamu na sio kifo.

Hatua za awali mwigulu alizozifanya ni kwenda gereza la Geita mjini alikohifadhiwa kijana huyo kwa madai ameshitakiwa na mwajili wake kwa kosa la wizi lililopelekea yeye kupigwa.
Katika mahojiano ya waziri Mwigulu Nchemba na kijana huyo,Mwigulu alibaini kuwa kijana huyo aliyepo gerezani ndiye mhanga wa tukio lile kwa uthibitisho wa makovu yaliyopo mwili mwake na mavazi aliyovalia wakati anateswa na wakati yupo hapo gerezani.

Katika hali hiyo ilimlazimi Mh.Mwigulu kwenda mgodini akiwa ameambatana na kijana huyo kwaajili ya kutambua waliofanya vitendo hivyo vya kinyama.Katika oparesheni hiyo, kijana  aliyeteswa na kujeruhiwa aliwabaini watanzania 5 ambao ni walinzi wa eneo hilo na mchina mmoja walioshirikiana kumpiga,kumtesa na kumjeruhi.

Kufuatia utambuzi huo na maelezo ya wahusika,Nchemba akaagiza wahusika wakamatwe mara moja na ameondoka nao kwa hatua zaidi za kisheria.

Katika hali nyingine ya kusikitisha,Mwigulu amebaini uwepo wa wahamiaji haramu raia wa china katika mgodi huo ambapo nyaraka za uhamiaji mkoa wa geita zinainesha raia 28 wenye vibali ndio waliruhusiwa kukaa kwenye mgodi huo,lakini katika operasheni ya kushitukiza aliyoifanya Mh.Mwigulu nchemba amebaini uwepo wa raia wa china zaidi ya 50 wanaoishi katika mgodi huo kinyume na sheria.Hivyo amemuagiza mkuu wa mkoa na timu yake ya uhamiaji kuhakikisha wote wasio na vibali wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania