CURRENT NEWS

Friday, August 5, 2016

JAJI WA FAILI LA UKATILI MKUBWA ZAIDI WA KINGONI UINGEREZA AJIUZULUA


Jaji aliyekuwa akishughulikia faili kubwa zaidi la unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto nchini Uingereza amejiuzulu na kuwa jaji wa tatu kung'atuka tangu uchunguzi wa kesi hiyo ulipotangazwa miaka miwili iliyopita.
Jaji Lowell Goddard amejiuzulu bila ya kutoa maelezo yoyote, mwaka mmoja tu baada ya kushika wadhifa huo wa kuchunguza na kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kihistoria wa kingono dhidi ya watoto na jinsi ulivyokuwa ukifichwa nchini Uingereza.
Mwathirika wa ukatili wa kingono Uingereza
Uchunguzi huo huru ulianzishwa mwaka 2014 kwa ajili ya kuchunguza miongo ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto katika taasisi za umma na za watu binafsi nchini Uingereza.
Kesi ya unyanyasaji wa kingoni dhidi ya Lord Greville Janner imepangwa kuanza Machi mwakani na kuendelea hadi mwishoni mwa mwezi May. Janner alikuwa mwanasiasa wa Uingereza, mwanasheria na mwandishi na inasemekana kuwa, aliwanyanyasa kingoni watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Mwanasiasa huyo Myahudi alifariki dunia kabla ya mahakama kuweka wazi ukweli wa mambo kuhusu tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Mtoto aliyefanyiwa ukatili wa kingoni
Kujiuzulu kwa jaji wa faili la unyanyasaji mkubwa zaidi wa kingono dhidi ya watoto nchini Uingereza kumekuja baada ya kufichuliwa takwimu za kutisha kuhusu unyanyasaji wa watoto huko England na Wales. Ofisi ya Taifa ya Takwimu imefichua kwamba, mtu mzima mmoja kati ya kila 14 alifanyiwa ukatili wa kingoni katika kipindi cha itotoni mwake huko Uingereza.
Vilevile matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa wanawake zaidi ya nusu milioni na wanaume zaidi ya laki moja walinyanyaswa kingoni ama kwa kubakwa au aina nyingine za ukatili wa aina hiyo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania