CURRENT NEWS

Wednesday, August 3, 2016

KOREA KASKAZINI YAFYATUA KOMBORA LINGINE

Korea Kaskazini imefanya majaribio ya makombora ya masafa marefu mashariki mwa pwani ya nchi na kuzua shtuma za kimataifa.
Korea Kusini inasema kuwa hiyo ilionyesha tamaa ya Korea Kaskazini kushambulia majirani zake.
Japan inasema kuwa kombora hilo lilianguka katika bahari ya Japan.
Waziri mkuu Shinzo Abe ametaja kitendo hicho kuwa cha uchokozi na tishio kubwa kwa usalama wa Japan.
Marekani inasema kuwa makombora mawili yalifyatuliwa lakini moja likalipuka muda mfupi baada ya kufyatuliwa .
Inasema kuwa iko tayari kujilinda pamoja na washirika wake.
Jaribio hilo ndilo la hivi punde linalokiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania