CURRENT NEWS

Wednesday, August 10, 2016

MARUFUKU MABWANA NA MABIBI SHAMBA KILOLO KUKAA OFISINI - DC ASIA

Mkurugenzi  wa Halmashauri  ya  Kilolo Bw Aloyce Kwezi akiwa na mkuu  wa  wilaya ya Kilolo Bi Asia Abdalah katika  viwanja  vya nane  nane    jijini Mbeya  mara  baada ya waziri  mkuu kumaliza  kufunga maonyesho  hayo

 Na MatukiodaimaBlog


SERIKALI  ya  wilaya  ya Kilolo  mkoani Iringa imewaagiza mabwana na mabibi  shamba katika  halmashauri  hiyo kutoka  maofisini  na kwenda  mashambani  kuwasaidia  wakulima kulima  kisasa  ili  kuongeza uzalishaji wa mazao.

Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Bi Asia Abdalah aliyasema  hayoa wakati  wa kilele  cha maonyesho  ya   wakulima (nane  nane )   kwenye  banda  ya Halmashauri  ya  wilaya  ya  Kilolo  wakati  wa  kufunga maonyesho  hayo juzi.

Alisema kuwa  pamoja na wilaya  yake  kuonyesha ushiriki mzuri  wa maonyesho hayo na wananchi  wengi  kufika  kujifunza katika banda  la  Kilolo namna ya  kilimo bora  chenye  tija  ila alisema  bado  wao kama  Kilolo kwa  kushirikiana na mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw , Aloyce Kwezi  pamoja na  wataalam  wote hasa  wale  wa  kilimo kufanya kazi kama  timu  ili  kuwasaidia  wakulima wa  Kilolo kusonga mbele 

Mkuu  huyo  alisema kuwa kati ya  wilaya  zinazoongoza  kwa  kilimo  cha mahindi  na mazao mengine ya  biashara  ndani ya  mkoa  wa Iringa  ni pamoja na wilaya  hiyo ya  Kilolo hivyo alisema iwapo  kila mtaalam  wa  kilimo atawajibika kwa nafasi  yake kauli mbiu ya Rais Dr  John Magufuli ya Hapa  Kazi  tu  inaweza  kuwasaidia   wananchi  kuongeza kasi ya uzalishaji .

Kwani alisema  pamoja na  jitihada  kubwa  zinazofanywa  na  wataalam  hao  wa  kilimo katika  wilaya ya  Kilolo katika  kuwasaidia  wakulima ila bado zipo  changamoto kiasi  kwa  baadhi ya wataalam  wa  kilimo  kutotimiza  wajibu  wao .

“ Lengo  ni  kuona  kila bwana  shamba ama  bibi shamba kwa maana ya wataalam wa ugani  wote  wanatimiza wajibu  wao  kwa kutoka maofisini na kwenda mashambani  walikowakulima  ili  kuwasaidia  kuongeza kasi ya  uzalishaji zaidi”

Hata  hivyo  alisema iwapo  wataalam  wa  kilimo watakwenda  kwa  wananchi na kushinda nao mashamani upo  uwezekano  wa wilaya ya  Kilolo  kwa maonyesho yajayo  kushika nafasi ya kwanza kikanda na kuwa na wakulima wenye kasi kubwa ya  uzalishaji .

Pia  alisema moja kati ya majukumu  ambayo yametolewa na  waziri  mkuu  wakati wa ufungaji wa maonyesho hayo  ni pamoja na  kusimamia kasi  ya uzalishaji na  kuwa  kwa  wilaya ya  Kilolo suala   hilo linawezekana kusimamiwa na  kufanikiwa kwa kiasi  kikubwa .

Huku kwa  upande  wake Mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri ya  Kilolo  Bw Aloyce Kwezi   alisema kuwa wilaya   hiyo iaongoza kwa  kilimo  cha nyanya ,vitunguu na mahindi pamoja na mazao  mengine na  kuwa uwezekano  wa wananchi wa Kilolo  kufanikiwa  kiuchumi  upo  mkubwa iwapo  kila mmoja  atatimiza  wajibu  wake .
Alisema zao  la nyanya  limekuwa ni ukombozi  mkubwa kwa wananchi  wa Ilula kama  ilivyo zao la vitunguu  kwa  waanchi wa Nyanzwa na  kudai hadi  sasa  serikali imeendelea  kuwasaidia  wakulima hao katika kuboresha skimu  za  umwagiliaji katika maeneo ya Mtandika , Ruaha mbuyuni na Nyanzwa na  kuwa  kupitia skimu  hizo  wananchi  wameweza  kuongeza uzalishaji .
MWISHO
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania