CURRENT NEWS

Thursday, August 4, 2016

MAUAJI YA WANAWAKE YAKITHIRI CANADA

Canada imezindua uchunguzi wa hali ya juu dhidi ya ongezeko la viwango vya juu vya mauaji na kupotea kwa wanawake na wasichana wenye asili ya nchi hiyo,suala ambalo limevuta hisia za mataifa kuikosoa nchi hiyo .
Waziri wa mambo ya ndani wa Canada, Carolyn Bennett, ameitisha uchunguzi unaoelezwa kuwa ni wa kihistoria kuwahi kufanyika, akisisitiza haja ya kuendesha uchunguzi ili kujua chanzo cha vurugu hiyo, na kueleza kwamba moja ya sababu zinazosababisha hali hiyo ni pamoja na ubaguzi wa rangi,unyanyasaji wa kijinsia na kile alichokiita athari endelevu za ukoloni.
Miaka miwili iliyopita , Polisi wa Canada waliarifu yakwamba kulikuwa na kesi zaidi ya elfu moja zilizofunguliwa za vifo vya wazawa wanawake na wasichana wazawa kati ya mwaka 1980 na 2012. Uchunguzi dhidi ya kesi za namna hiyo unatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi ujao wa September na mwenendo wa kesi hizo unatarajiwa kuhusisha mashahidi, ingawaje si kuwapa dhima ya jinai.
Kwisha kwa kesi hizo kunatarajiwa kuja na majumuisho ya uchunguzi huo na nini walichogundua na kutoa ripoti kamili mnamo mwishoni mwa mwaka 2018.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania