CURRENT NEWS

Sunday, August 7, 2016

OSCAR PISTTORIUS AJERUHIWA GEREZANI

Maafisa wa magereza nchini Afrika Kusini, wanasema kuwa mwanariadha mlemavu wa nchi hiyo Oscar Pistorius, ametibiwa hospitalini baada ya kupata majeraha akiwa korokoroni.
Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chakeImage copyrightAFP
Image captionMsemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chake
Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chake, lakini kwa sasa amerejeshwa gerezani anakohudumia kifungo cha miaka sita kwa kosa la kumuuwa mpenziwe wa kike Reeva Steenkamp.
Kuna ripoti inayosema kuwa alikuwa amejeruhiwa kwenye kifundo cha mkono.
Kumeibuku uvumi katika mitandao ya kijamii nchini Afrika Kusini kuwa Pistorius alikuwa amejaribu kujitia kitanzi lakini hilo limekanushwa na familia ya mwanariadha huyo.
Reeva SteenkampImage copyrightEPA
Image captionReeva Steenkamp
Mwezi uliopita, waendesha mashtaka nchini Afrika Kusini, walisema kuwa watakata rufaa kupinga hukumu ya miaka sita ya Pistorius, wakisema kuwa ni hukumu ndogo mno.
Mwanariadha huyo alimuuwa mpenziwe wa kike , kwa kumpiga risasi nyumbani kwake wakati wa siku kuu ya wapendanao mnamo mwaka wa 2013, akisema kuwa alidhania ni mwizi
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania