CURRENT NEWS

Wednesday, August 10, 2016

PROFESA MBARAWA:SERIKALI IMEJIPANGA KUONDOA MSONGAMANO KATIKATI YA JIJI

Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizinduwa safari za gari moshi jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita wakiwa katika usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari zake zimezinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akipanda katika gari moshi ambalo safari zake zimezinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika usafiri wa gari moshi hilo ambalo safari zake zimezinduliwa jana jijini Dar es Salaam. 
Wananchi wakiwa katika usafiri wa gari moshi uliozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
Safari ikiwa inaendelea katika mabehewa na baadhi ya watendaji wa TRL gari moshi kati ya Pugu jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
Safari inaendelea
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa akizungumza katika uzinduzi wa Treni ya Pugu hadi Stesheni jana jijini Dar es Salaam. 
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza juu huduma ya usafiri wa reli kwa wananchi wa Pugu jana katika uzinduzi wa Treni ya Pugu hadi Stesheni jana jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa Treni ya Pugu hadi Stesheni jana jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano , Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanakuwa na usafiri wa uhakika katika kuondoa msongamano wa magari mjini kwa kutumia usafiri wa gari moshi. 

Hayo ameyasema jana Profesa Mbarawa wakati wa uzinduzi wa gari moshi linalofanya safari zake kuanzia Stesheni hadi Pugu, amessema kuwa kuanza kwa usafiri huo umepunguza daladala 45. 

Amesema kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha inapungaza kama sio kumaliza kabisa msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Profesa Mbarawa amesema kuwa katika hatua nyingine wanaangalia usafiri kwa njia ya boti katika baadhi ya maeneo na wataalam walishafanya kazi hiyo. 

Aidha amewataka wafanya kazi kuacha kufanya kazi kwa mazoea kama walivyokuwa wakifanya na watakaofanya hivyo hawatavumiliwa ikiwa ni pamoja na kufisadi mali za reli. 

Hata hivyo amesema waliojenga katika miundombinu ya reli wanatakiwa kubomolewa kwani kuwepo kwa nyumba hizo katika miundombinu hiyo ni kosa kisheria .Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wakazi wa Dar es Salaam kuwa wataondokana na foleni kutokana na jitihada mbalimbali. 

Amesema moja jitihada hizo ni kuondoa malori ya mafuta ambapo mafuta yatasafirishwa kwa njia ya bomba mpaka Chalinze na kuanza kwa safari ya mikoani. Meya wa Jiji, Isaya Mwita amewataka wananchi kutumia usafiri huo kutokana na kutokwa na foleni na gharama yake kuwa nafuu. 

Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa usafiri wameanza kutokana na nguvu ya serikali kuwa karibu katika utoaji wa huduma ya usafiri huo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania