CURRENT NEWS

Wednesday, August 10, 2016

TRUMP AZUA MJADALA TENA MAREKANI

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amezua mjadala mpya baada ya kuwahimiza wafuasi wake wenye bunduki kumzuia mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton, kubatilisha haki yao ya kikatiba ya kumiliki silaha.
Bw Trump alikuwa akihutubu katika mkutano wa siasa katika jimbo la North Carolina.
Bw Trump alikuwa amesema kwamba iwapo Bi Clinton atashinda basi atateua majaji wa Mahakama ya Juu ambao watafanikisha kuondolewa kwa haki ya raia kumiliki bunduki.
Alidokeza kwamba ni hatua ya raia pekee, ambayo inaweza kuzuia hilo lisifanyike.
Maafisa wa kampeni wa Clinton wameshutumu matamshi ya Trump na kusema ni hatari.
Lakini washauri wake wamesema alikuwa tu anawahimiza watu wanaoamini katika haki ya raia kumiliki silaha watumie kura zao kufanya uamuzi.
BBC.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania