CURRENT NEWS

Wednesday, August 10, 2016

WACHEZAJI WA KOREA KASKAZINI NA KUSINI WAPIGA SELFIE

Wanamichezo wa mazoezi ya viungo kutoka Korea Kusini na Kaskazini, ambao wanashiriki Michezo ya Olimpiki Rio 2016, wameuonesha ulimwengu ishara ya umoja, kwa kupiga selfie pamoja.
Lee Eun-ju wa Korea Kusini na Hong Un-jong wa Kaskazini walipiga picha wakiwa wametabasamu wakati wa mazoezi kabla ya kuanza kwa michezo hiyo.
Picha za wanawake hao wawili zimesifiwa sana kwa kuashiria moyo wa Olimpiki wa kuwaleta watu pamoja.
Korea Kaskazini na Kusini huwa na uhasama mkubwa.
Uhusiano baina ya nchi hizo mbili umedorora hata zaidi, kutokana na hatua ya karibuni ya Pyongyang kufanyia majaribio makombora.
Lee Eun-ju, kushoto, azungumza na Hong Un Jong wa Korea KaskaziniImage copyrightAP
Image captionWanamichezo hao walikutana wakati wa raundi ya kufuzu kwa mashindano kamili tarehe 7 Agosti
Lee Eun-ju na Hong Un JongImage copyrightAP
Image captionWanamichezo wote wawili hawakufanikiwa kufuzu, lakini bila shaka walibeba 'dhahabu' ya uanadiplomasia
Picha bora zaidi Olimpiki?
"Hii ndiyo maana huwa twashiriki Olimpiki," mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Ian Bremmer aliandika kwenye Twitter na kuweka picha hiyo.
Ujumbe wake ulisambazwa zaidi ya mara 18,000.
Wengine hata hivyo hawakufurahishwa na hilo.
"Anaruhusiwa kufanya urafiki na adui?", mmoja wa watu mitandaoni waliuliza, na wengine wakaeleza wasiwasi kwamba huenda Hong akaadhibiwa akirejea nyumbani.
Lee, 17, na Hong, 27, wote walishiriki kama wachezaji wa kufuzu wakiwa binafsi. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Lee kushiriki michezo ya Olimpiki.
Lee Eun JuImage copyrightREUTERS
Image captionLee akishiriki kwenye mashindano ya Olimpiki Rio
Hong Un Jong uwanjani RioImage copyrightAP
Image captionHong akishiriki mashindano ya Rio tarehe 7 Agosti. Alikuwa mwanamichezo wa kwanza wa mazoezi ya viungo kushindia taifa lake nishani, aliposhinda Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008.
Wengi walieleza tofauti iliyopo baina ya wanawake hao wawili na timu ya Olimpiki ya Lebanon iliyokataa kuabiri basi moja na wanamichezo wa Israel.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania