CURRENT NEWS

Friday, August 5, 2016

WAPIGANIA UHURU WA PALESTINA WAPINGA UHUSIANO NA ISRAEL


Makundi ya kupigania uhuru wa Palestina yamepinga hatua zinazochukuliwa na baadhi ya nchi za Kiarabu za kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel unaendelea kukalia wka mabavu ardhi tukufu za Palestina.

Taarifa iliyotolewa na makundi hayo imesema, kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel ni kinyume na mafundisho ya Uisalmu na matukufu ya Palestina na kwamba hatua hiyo itahalalisha mauaji yanayoendelea kufanywa na Israel dhidi raia wasio na hatia hususan wanawake na watoto wadogo. 
Ahmad Mudallal ambaye ni miongoni wma viongozi wa ngazi za juu wa harakati ya Juhad Islami ya Palestina amelaani hatua ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Emirates) na Pakistan wa kufanya mazoezi ya kijeshi na Israel na kusisitiza kuwa hatua hiyo imechukuliwa katika mikakati yakuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu. 
Hassan Mansour ambaye ni miongoni wma viongozi wa Harakati ya Wananchi kwa Ajili ya Ukombozi wa Palestina amesema kushiriki kwa Imarati na Pakistan katika mazoezi ya kijeshi na Israel kunapingana na matukufu ya Kiislamu na malengo ya Wapalestina. 
Gazeti la Haaretz la Israel limefichua kwamba nchi za Pakistan, Marekani, Uhispania na Imarati zitashirikiana na Israel katika mazoezi ya kijeshi yatakayofanyika wiki mbili zijazo katika jimbo la Nevad nchini marekani
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania