CURRENT NEWS

Tuesday, September 27, 2016

MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA LUNINGA


Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) Bw. Sevelin Mushi wa kwanza kulia akimkabidhi ungo wa king’amuzi cha azam  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano  MNH, Aminiel Aligaesha kushoto  kwa ajili ya wodi ya wazazi wakati wa hafla fupi ya kuchangia damu katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) Bw. Sevelin Mushi wa kwanza kulia akimkabidhi luninga  Afisa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano  MNH, Aminiel Aligaesha kushoto  kwa ajili ya wodi ya wazazi wakati wa hafla fupi ya kuchangia damu katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) Bw. Marceli mushi akichangia damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakati wa hafla fupi ya kuchangia damu katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) Bw. Sevelin Mushi akichangia damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakati wa hafla fupi ya kuchangia damu katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.

Wanachama wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) wakisubiri kuchangia damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakati wa hafla fupi ya kuchangia damu katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.


 Picha Na Ally Daud.
 Na Sheila Simba

Wanachama wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) wametoa luninga moja,deki,na king’amuzi cha azam katika Hosptali Ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya wodi ya wazazi pamoja na kuchangia damu.


Akizungumza wakati wa kutoa televisheni hiyo pamoja kuchangia damu Mwenyekiti wa umoja huo  Marceli mushi , amesema kuwa atawaamasisha vikundi vingine kuchangia katika huduma za afya ili kusaidia watanzania wengine wenye mahitaji.


“Tumekuja hapa tumejifunza mengi na tumepata elimu huko kwenye jamii tunakoenda kukutana na watu tutafikisha ujumbe ili nao waweze kujitolea kuchangia kuokoa maisha ya watu”,alisema Mushi


Kwa upande wake  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano  MNH, Aminiel Aligaesha ameshukuru  umoja huo kwa kujitolea kuchangia damu na kutoa luninga hiyo itakayo tumika kutoa elimu kwa kinamama


“Tunashukuru kwa kweli kwasababu mahitaji ya damu ni makubwa hasa kwa kina mama wajawazito na watoto na tunatumia chupa 90 mpaka 110 kwa siku”,alisema Aligaesha

Naye Kaimu Meneja wa wodi hiyo Bi Stella Medadi amesema luninga hiyo itatumika  kwa kuweka vipindi vitakavyosaidia kutoa elimu ya uzazi,lishe na maandalizi ya mama mjamzito pamoja na vidokezo vya hatari kwa mama. 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania