CURRENT NEWS

Sunday, September 18, 2016

BOTI ZA KIVITA ZA IRAN ZAZITIA KIWEWE MELI ZA KIVITA ZA MAREKANI


Boti za kivita za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC zimezitia kiwewe na kuzidhalilisha meli za kivita za Marekani katika eneo la Ghguba ya Uajemi.
Hayo yamesemwa na Meja Jenerali Mohammad Hossein Baqeri Mkuu wa Vikosi Vyote vya Ulinzi vya Iran alipokuwa akihutubia makamanda wa jeshi la SEPAH (IRGC) hapa mjini Tehran jana Jumamosi.
Ameongeza kuwa, "Vitendo vya kishujaa vya vikosi vya majini vya IRGC vimezidhalilisha meli za kivita za Marekani katika Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormuz." Ameongeza kuwa boti za kasi za jeshi la SEPAH zimezitia kiwewe meli za kivita za Marekani.

Meja Jenerali Baqeri


Mwezi huu wa Septemba msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, Kapteni Jeff Davis alisema boti saba za kasi za wanamaji wa IRGC ziliiandama meli ya kivita ya Marekani ya USS Firebolt Septemba sita baada ya meli hiyo ya Marekani kukaribia kuingia kwenye maji ya Iran.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania