CURRENT NEWS

Wednesday, September 14, 2016

DC STAKI APONGEZA JAMII YA KIMASAI KUACHANA NA MILA POTOFU NA KUANZA KUMWABUDU MUNGUMkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akisikiliza kwa makini maelezo ya mmoja ya wazee wa kabila la Kimasai kuhusu umuhimu wa elimu katika maeneo hayo
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule, Viongozi wa dini na wananchi wakishuhudia sherehe ya vijana wa kimasai (Morani) kuingia stage ya uzeeni
 Baadhi ya vijana wa Kimasai wakipandisha Mori kwa furaha ya kuingia stage ya uzee

Dc Staki akisalimiana na viongozi wa dini walioendesha misa hiyo mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo
 Dc Staki akishuhudia vijana wakipandisha Mori
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule akiwa kwenye sala wakati wa Misa
Dc Staki akifatilia kwa makini zoezi la kuingia hatua ya Uzee kwa waliokuwa vijana wa Kimasai
 
Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule amewapongeza baadhi ya vijana wa kimasai kwa kuachana na imani potofu na hatimaye kuanza kumwabudu Mungu kwa kuhudhuria Misa mbalimbali katika makanisa.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu huyo wa Wilaya hiyo wakati wa sherehe maalumu kwa waliokuwa vijana wa Kimasai (Morani) kuingia hatua kubwa ya uzeeni na ya heshima katika kabila hilo.

 Sherehe hiyo ilifanyika katika uwanja wa Kitongoji cha Endevisi, Kijiji cha Emuguru na ibada hiyo kuongozwa na Mchungaji Joshua Laiser kutoka kanisa la Kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) Wilaya ya Hai Dayosisi ya Moshi na Mchungaji Andrea Sangolo wa Usharika wa Bonde la Ruvu Same na baadaye kufuatiwa na shughuli za kutoa Baraka kwa vijana hao zoezi lililofanywa na viongozi wa dini, Serikali na Wazee wa Mila.

Sherehe hizo zimefanyika zikiwa na lengo la kufanya mageuzi kwa jamii ya kimasai na hatimaye kuachana na mila potofu kama vile kuabudu waganga wa jadi na kuanza kumuabudu Mungu wa kweli.

Pamoja na pongezi hizo za mkuu wa Wilaya ya Same kwa jamii ya kimasai kufanya mapinduzi hayo ya kuachana na mila potofu pia aliwataka kuwekeza zaidi kwenye swala la elimu na kuwataka kuwaruhusu watoto wote wa kiume na watoto wa kike kusoma kwa usawa.

Katika Jamii ya kimasai kumekuwepo na kadhia mbalimbali za mila Potofu za kuozesha watoto wadogo na kufanyiwa tohara kwa watoto wa kike, matukio ya ubabe ikiwemo wizi wa mifugo na mauaji kwa imani potofu jambo ambalo limezuiwa na Mkuu huyo wa Wilaya hiyo.

Dc Staki ametumia nafasi hiyo pia kuwataka wananchi wote wa jamii hiyo ya Kimasai kutumia rasilimali walizo nazo kwa kuuza kiasi ikiwemo Ng’ombe ili kujenga Hospitali zitakazo wasaidia kuimarisha afya zao na kujenga shule ambazo zitawaimarisha watoto wao kielimu.

Tukio hilo la Ibada kwa vijana hao ni kubwa katika historia ya kabila la Kimasai na limejumuisha jamii ya Kimasai kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Tanzania na nchi jirani ya Kenya.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania