CURRENT NEWS

Sunday, September 18, 2016

KAMPUNI YA ASAS IRINGA YAPONGEZWA KWA KUJITOLEA MIRADI YA ZAIDI YA TSH MILIONI 400 HOSPITALI YA MKOA

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza (kushoto)  akimpongeza Salim Asas   (kulia) mara  baada ya  kuweka  jiwe la msingi katika miradi  mikubwa  miwili iliyofadhili   kampuni ya Asas ukiwemo  mradi wa jengo la  kituo cha  damu  salama Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa na jengo la  watoto  wanaozaliwa njiti yote yaliyofadhiliwa kwa zaidi ya Tsh milioni 400  na  kampuni hiyo ya  Asas ya  mkoa wa Iringa(picha na matukiodaimaBlog )
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  akisaini kitabu cha  wageni
Mkurugenzi wa kampuni ya  Asas ya  Iringa wa  tatu kushoto  akiwa katika Hafla  hiyo
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza akitoa  hutuba yake ya ufunguzi wa miradi hiyo
Damu  iliyochangiwa
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza ( wa  tano  kulia ) akiwa na mfadhiliwa wa  miradi ya jengo la  kituo cha  damu  salama Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa Salim Asas kutoka  kampuni ya  Asas ya  mkoa wa Iringa (kulia kwake) pamoja na viongozi  wengine walioshiriki Halfa ya  uwekaji wa mawe ya msingi katika mradi  huo  na jengo la  watoto njiti yote  ikiwa na  zaidi ya Tsh milioni 400 zilizotolewa na kampuni ya Asas wa  nne  kutoka  kushoto ni mkuu wa  wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela
Mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  akizindua  majengo hayo  kwa  hotuba
Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza na mfadhili wa  miradi ya  jengo la Benki ya  damu na jengo la watoto  njiti wakiweka jiwe la msingi leo anayeshuhudia ni mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard  Kasesela
Mkuu wa  mkoa wa Iringa  akiwa ndani ya jengo la benki ya  damu
Viongozi mbali mbali wakiwa na mkuu wa mkoa kukagua  kituo hicho
Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza ( wa  nne   kulia ) akiwa na mfadhiliwa wa  miradi ya jengo la  kituo cha  damu  salama Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa Salim Asas kutoka  kampuni ya  Asas ya  mkoa wa Iringa (kulia kwake) pamoja na viongozi  wengine walioshiriki Halfa ya  uwekaji wa mawe ya msingi katika mradi  huo  na jengo la  watoto njiti yote  ikiwa na  zaidi ya Tsh milioni 400 zilizotolewa na kampuni ya Asas wa  nne  kutoka  kushoto ni mkuu wa  wilaya ya  Iringa  Richard  Kasesela


                                                                Na MatukiodaimaBlog
SERIKALI  ya  mkoa  wa  Iringa   imepongeza  msaada mkubwa uliotolewa na kampuni ya  Asas  ya  mkoa hapa wa ujenzi wa jengo la  kituo  cha  damu  salama  cha  kisasa na ujenzi wa  jengo la  watoto  wanaozaliwa  njiti katika  Hospitali  teule ya  mkoa  wa  Iringa pamoja miradi  itakayogharimu zaidi ya  Tsh  milioni 400

Katika  taarifa   iliyosomwa na mganga  mkuu  wa  Hospitali ya rufaa ya  mkoa wa Iringa Dr Robert salim wakati wa  hafla ya  uwekaji wa jiwe la msingi   katika miradi hiyo leo  mbele ya mgeni rasmi   mkuu wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza  alisema  kuwa awali  uongozi wa hospitali  hiyo  ulimwandikia  barua  mfanyabiashara    huyo  ili  kusaidia  msaada wa kontena ambalo  lingetumika katika  kituo cha benki ya  damu salama ila mfanyabiashara   huyo alijitolea  kujenga jengo  hilo la  kisasa na kuongeza msaada wa jengo la watoto  wanaozaliwa  njiti .

“Kutokana na agizo la Serikali la kuanzisha Benki za damu salama katika Mikoa..... Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Mfadhili  Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS iliona ni vyema kujenga jengo la Kituo Kidogo cha damu salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ili kufikia azma hiyo. ...Hospitali ilimuomba Mfadhili huyo atoe msaada wa “Container” kwa ajili ya shughuli hiyo, lakini Mfadhili kwa kuona umuhimu wa huduma ya damu salama katika Mkoa aliomba apewe ramani ili ajenge kituo hicho badala ya kutumia“Container”.”alisema


Dr Salim alisema  kuwa Hospitali   hiyo kabla ya  mfanyabiashara   huyo  kujitolea  ujenzi wa  jengo  hilo  kituo cha  kidogo  cha damu  salama  ulikuwa  ukitegemea  damu  kutoka  kituo  cha kanda  kilichopo  mkoani  Mbeya  ila  sasa  wataweza  kukusanya  damu  kupitia  kituo  hicho.

Alisema  kuwa lengo la mradi huu ni Kuboresha upatikanaji wa huduma za damu salama katika Mkoa wa Iringa kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya damu salama katika Vituo vya kutolea huduma za afya na kupunguza vifo vya Uzazi, Watoto wachanga, Watoto na Wahanga wa ajali za barabarani na kuwa lengo la Mkoa kwa mwezi ni kukusanya chupa 784 na kwa mwaka ni chupa 9,413 (units).

Hata  hivyo  alisema mahitaji ya damu kwa mwezi katika Mkoa ni chupa 700 (unit) na katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ni chupa 160-200 Units kwa mwezi kuwa tangu kituo kianze kutumika mwezi Februari,2016 Mkoa umekusanya chupa 2,065 (22%) hadi sasa.

“Tunakushukuru mkuu wa mkoa  kwa kukubali mwaliko wetu wa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla hii ya kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mfadhili wetu Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS ya Iringa. Katika hafla hii fupi tutakuomba uweke jiwe la Msingi katika Mradi wa jengo la Kituo Kidogo cha Damu Salama na Jengo la Wodi ya Watoto wachanga vyote  vikiwa ni  hisani  kutoka kwa mfadhili wetu  Salim F Abri “


Alisema kuwa ujenzi huo  unafanywa namkandarasi anayenga mradi huu ni Buyungu General Enterprise wa Iringa chini ya usimamizi wa  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye amechangia kuchora ramani za jengo hili na kusimamia mradi mpaka ulipokamilika, mchango wake kama angelipwa ni Tshs.13,939,200.00.

Na kuwa  utekelezaji wa mradi ulianza kutekelezwa mwezi Novemba, 2014 na umekamilika mwezi Agosti, 2015. Jengo limeanza kutumika mwezi Februari, 2016. Pamoja na kujenga jengo hili Mfadhili pia ametoa msaada wa samani, mafriji makubwa 4 ya kutunzia damu na Computer 1 wenye thamani ya Tshs.30,000,000.00.
`
Aidha, Hospitali ya Vicenza ya Nchili Italia ilichangia Tshs. 800,000.00 kwaajili ya kusafisha eneo la ujenzi na Meneja wa Benki ya Damu Salama ya Kanda Mbeya ametoa msaada wa Vitanda 2 vya kutolea damu, Mizani (weighing scales) za kupimia uzito chupa za damu na Mzani 1 wa kupimia watu wanaojitolea damu.

Alisema Mpaka umekamilika mradi huu wa kituo  cha damu  salama umegharimu jumla ya Tshs.154,880,000.00 bila samani na vifaa tiba kuwa  faida kuwa ya mradi huo uboresha utoaji wa huduma  za damu salama kwa kuwa na eneo kubwa la kufanyia kazi,Kupunguza malalamiko ya wananchi kwa kukosa damu salama
Pia Kuzuia maambukizi ya magonjwa ya VVU/UKIMWI, Hepatitis B na C na Kaswende,Kupunguza vifo vya uzazi, watoto wachanga, watoto na wahanga wa ajali vinavyotokana upungufu wa damu au kutokwa na damu nyingi,Kupunguza gharama za kufuata damu salama umbali mrefu (Damu salama Kanda Mbeya) na  kuongeza  kuwa Wanufaika zaidi ni
Watoto, Watoto wachanga, Mama wajawazito, Wahanga wa ajali za barabarani na jamii kwa ujumla.

Dr Salim alisema kupitia mradi huo wanategemea Kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya huduma isiyoridhisha ya damu salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na Halmashauri na kukomesha tatizo la rushwa.

Kuhusu mradi wa jengo la watoto wanaozaliwa njiti alisema kuwa Mpaka utakapokamilika mradi huu unatarajiwa kugharimu jumla ya Tshs.309,210,000.00 bila samani na vifaa tiba ambazo  zote fedha za mfadhili huyo kampuni ya  Asas.

Akizungumzia  hatua ya familia  yake  kujitolea  kujenga  miradi hiyo mikubwa Asas  alisema ni kutokana na changamoto kubwa  aliyoiona  baada ya  kutembelea  Hospitali hiyo na hata  mmoja kati ya  wanafamilia  wake  kupoteza mtoto  baada ya kuzaliwa njiti na kukosa chumba  kwa ajili ya  kunusuru uhai  wake.

Mkuu wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza pamoja na kupongeza kampuni ya Asas kwa kujitolea misaada  hiyo bado  aliomba  wahisani  wengine  kuzidi  kujitolea kwa ajili ya  maendeleo  na kuwa kama mkoa  unatambua mchango mkubwa wa kimaendeleo  unaofanywa na kampuni ya Asas  pia mfanyabiashara Rajan  aliyepata  kujitolea  kujenga  chumba cha kuhifadhia maiti  hospitalini hapo .

Awali  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  akimkaribisha mkuu wa mkoa  kuweka mawe ya msingi katika  miradi  hiyo  alisema misaada anayoendelea  kutoka Asas si  tu kwa CCM na serikali yake  ila hata kwa  vyama  vya  upinzani na  wakazi mbali mbali wa mji  wa Iringa hivyo kutaka Halmashauri ya Manispaa  kutunza  miradi hiyo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania