CURRENT NEWS

Friday, September 9, 2016

LEO NI LEO MISS ILALA 2016 JIJINI DAR ES SALAAM

Washiriki wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha baada ya mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. warembo hao wanataraji kupanda jukwaani Septemba 9, 2016 katika Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro
 Warembo wa Miss Ilala 2016 wakiwa katika picha ya pamoja.
**************

SHINDANO la Kumsaka Miss Ilala 2016 linafanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

Mbali na kufanyika kwa shindano hilo pia litatumika kuadhimisha miaka 20 ya shindano la Miss Ilala tangu kuanza kufanyika kwake na warembo mbalimbali waliowahi kushiriki na kushinda taji hilo watahudhuria.

Mratibu wa shindano hilo, Erick Othman kutoka Kampuni ya Gogetime Enterprises ya jijini Dar es Salaam, alisema kuwa warembo 14 watapanda jukwaani kuwania taji hilo pamoja na tiketi ya kushiriki shindano la Kitaifa la Miss Tanzania 2016 linalotaraji kufanyika baadae mwaka huu.

Othman alisema mgeni rasmi katika shindano hilo leo hii ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, huku burudani ikitolewa na wasanii mbalimbali akiwepo Rubby.

Amewataja warembo wanaoshindana kuwania taji hilo kuwa ni Osmunda Mbeyela, Mercy Zephania, Melody Tryphone, Dalena David, Nuru Kondo, Julitha Kabete, Sporah Luhende, Queen Nazil, Lilian Omolo, Mariam Maabad, Brenda Allan, Sabrina Halifa, Agriphina Nathaniel na Grace Malikita.

Kwa upande wa zawadi za washindi, Kitundu alisema kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha sh milioni moja pamoja na portable TV kutoka Startimes, huku mshindi wa pili akipata sh 700,000 na kingamuzi, na mshindi wa tatu akipata sh 300,000 na kingamuzi pia.

Alisema kuwa mshindi wan ne atapata sh 200,000 na watano atapata sh 150,000 pamoja na kingamuzi huku warembo wengine watapata kifuta jasho cha sh 50,000.

Kiingilio katika shindano hilo ni Sh 50,000 kawaida na Sh 100,000 kwa viti maalum (VIP).

Wadhamini ni Coca cola, Atsko, Darling, Channel 10, Kitwe General Traders, Uefa Goo, Mustafa Hassanali, Majira, High Spirit, StarTimes, Father Kidevu Blog na wengineo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania