CURRENT NEWS

Wednesday, September 21, 2016

MAHAKAMA ZASHAURIWA KUZINGITIA HAKI YA MSINGI

Na.Sheila Simba-Maelezo
Mahakama nchini zimetakiwa kuzingatia haki ya msingi katika kutenda kazi,kuliko ufundi wa kisheria unaotumiwa na wanasheria katika kufanya kazi zao za kila siku.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar Es Salaam na Jaji Engera Kileo katika hotuba yake wakati wa hafla ya kumuanga iliyofanyika katika ofisi za Mahakama Kuu.

Amesema kuwa ni vyema haki itendeke kwa kila mtu ili kusaidia jamii kupata haki pale wanapokua na tatizo na kuongeza kuwa ni imani yake kuwa mwenye mamlaka ya kutoa uhai ni yule alikupa uhai pekee.

“Watoaji haki sio wote wamekamilika tunapoamua kutoa hukumu ya kifo unaweza kutoa kwa mtu ambaye hakutenda kosa hilo na kumuacha aliyefanya kosa”alisema Jaji Kileo

Aidha,ameeleza kuwa mahakama zinahitaji kusaidiwa katika kazi zake za uendeshaji wa kesi kwani ni gharama na wakati mwingine mahakama zinashindwa kutimiza wajibu wake kutokana na kushindwa kumudu gharama.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Othmani Chande, akizungumzia wasifu  Jaji Kileo amesema mahakama uadilifu na uaminifu wa Jaji huyo katika kipindi cha miaka 40 aliyoitumia sekta ya sheria nchini.

“kwa kweli Jaji Kileo amefanya kazi kubwa na anaondoka akiwa ametuachia urithi mzuri hasa wa kutumikia haki ya msingi katika kutenda haki na sio kuangalia ufundi wa kisheria kama ambavyo alivyokuwa anafanya kazi” alisema Chande

Ameongeza kuwa Jaji Kileo alikuwa ni mtu wa kuhakikisha kila  mtu anapata haki yake na kuheshimu haki na kusiitiza majaji wanawake kuiga mfano wake ili kusaidia mahakama kufanya kazi zake kwa kuzingatia maadili ya kazi.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania