CURRENT NEWS

Friday, September 23, 2016

MARAGA NDIO JAJI MKUU MPYA MTEULE WA KENYA

Jaji wa mahakama kuu jaji David Maraga ndio jaji mkuu mpya wa KenyaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionJaji wa mahakama kuu jaji David Maraga ndio jaji mkuu mpya wa Kenya
Jaji wa mahakama kuu nchini Kenya David Maraga ndio jaji mkuu mpya mteule wa Kenya.
David Maraga atachukua mahala pake Jaji mkuu mstaafu Willy Mutunga ambaye mda wake wa kuhudumu ulikamilika iwapo ataidhinishwa.
Jina lake litawasilishwa kwa rais Uhuru Kenyatta ili kuidhinishwa rasmi kabla ya kuwasilishwa mbele ya bunge ili kujadiliwa na kupitishwa.
Maraga mwenye umri wa miaka 64 aliwashinda wenzake 13 ambao pia walituma maombi yao ya kugombea wadhfa huo wa juu,akiwemo jaji wa mahakama ya juu Jacton Ojwang na Smokin Wanjala ,msomi Makau Mutua miongoni mwa wengine.
Majaji hustaafu wakiwa na umri wa miaka 70 hatua inayoaaminisha kwamba Maraga atahudumu kwa miaka sita.BBC
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania