CURRENT NEWS

Thursday, September 1, 2016

MNEC MUFINDI AWATAKA WANANCHI KUJIANDAA NA MILIONI 50 ZA RAIS DR MAGUFULI

                                                    Na MatukiodaimaBlog
WANANCHI  wilayani  Mufindi  mkoani  Iringa  wametakiwa  kuanza  maandalizi ya  kunufaika na milioni 50  kwa  kila  kijiji zilizopangwa  kutolewa na Rais Dr  John Magufuli kwa kuanza kujiunga  vikundi  vya  ujasiriamali na  kuvisajili  .

Wito   huo  umetolewa na  mjumbe  wa Halmashauri  kuu ya  Chama  cha mapinduzi (CCM)  Taifa kutoka wilaya ya  Mufindi ,Marcelina Mkini  wakati  akizungumza na  wanahabari  kuhusu utaratibu   huo mzuri  ulioahidiwa na Rais Dr  Magufuli  wakati wa kampeni .

Alisema  kuwa   ili  wananchi  kuweza  kunufaika na utaratibu   huo ni lazima   kujiunga katika  vikundi vya  watu  wenye  malengo  yanayofanana  na  kuvisajili  ili  pindi  pesa  hizo  zitakapotolewa  kuweza  kuzipata .

Mkini  alisema  kwa utaratibu wa  fedha  hizo  hazitatolewa  kwa  mtu  mmoja mmoja hivyo  kwa wale  ambao  wanazitamani  fedha  hizo  ni lazima  kuanza  kujiunga  katika  vikundi ambavyo vimesajiliwa .

" Lengo la  Rais   wetu  ni  kuona    wananchi   wananufaika na matunda  ya  nchi   hii ndio  sababu ya  kuahidi  kusaidia  vijiji fedha   hizo  shilingi  milioni 50 kwa  kila kijiji fedha  ambazo ni  nyingi  sana na  zitasaidia  wananchi  kujikwamua  katika  dimbwi la umasikini ........lazima  tumpongeze  sana kwa mtazamo  huu ambao  haujapata  kutokea "

Hivyo alitaka   vijana  ,wanawake na  wazee  kujiunga makundi  yenye malengo yanayofafa  yakiwemo ya  ufugaji kwa  wazee ama  kilimo na makundi  mengine  ambayo yatapelekea  vijiji   kuwa na vyama  vya  kuweka na  kukopa (SACCOS)  zao .

Mkini  ambae pia  ni  mwenyekiti  wa   umoja  wa  wanawake  Tanzania (CWT)  wilaya  hiyo ya  Mufindi  aliwataka  viongozi  wote  wa UWT   ngazi  zote  kusaidia  kuhamasisha  wanawake   kuonyesha mfano katika kuanzisha  vikundi  vya   uzalishaji mali .

Huku  akiwataka  kwa  kipindi   hiki  cha  kuelekea  kupata fedha   hizo  kuwa makini na matapeli  ambao  baadhi ya mikoa  wameanza   kujipitisha  kudanganya  wananchi  kuwa   fedha  hizo  zitapitia katika NGOs zao .
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania