CURRENT NEWS

Sunday, September 18, 2016

POWELL: ISRAEL IMEELEKEZA MABOMU 200 YA NYUKLIA UPANDE WA IRAN

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Colin Powell amekiri katika baruapepe zake kwa mmoja kati ya waitifaki wake wa kibiashara kwamba Israel ina makombora 200 ya nyuklia ambayo imeyaelekeza upande wa Iran.
Gazeti la Independet la Uingereza limefichua habari ya baruapepe iliyoandikwa na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Colin Powell akisema Israel ina makombora 200 ya nyuklia na kwamba yote yameelekezwa upande wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 
Kombora la nyuklia
Powell alituma baruapepe hiyo kwa mshirika wake wa kibiashara, Jeffrey Leeds ambaye pia ni mfadhili mkubwa wa chama Democratic, akizungumzia hotuba ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu katika Congresi ya Marekani akitahadharisha kuhusu makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi za kundi la 5+1. Powell alisema katika baruapepe hiyo kwamba Netanyahu hapendi kuona mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 yakizaa matunda. 
Colin Powell
Siku chache zilizopita mahaka (wadikizi) wa Russia waliingia katika akaunti ya aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Colin Powell na kuweka hadharani baruapepe zake. Baadhi ya baruapepe hizo zimetajwa kuwa zina taarifa nyeti na muhimu sana. 
IDHAA YA IRAN.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania