CURRENT NEWS

Wednesday, September 7, 2016

RAIS MAGUFULI ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA MABWENI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.  Prof. Joyce Ndalichako akipata maelezo ya awali kutoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Florens Luoga (wa kwanza kushoto) kuhusu ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati alipotembelea eneo la mradi huo muda mfupi kabla ya Rais kuwasili. Wa tatu kutoka Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.  Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maimuna Tarish akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga (wa kwanza kulia) kuhusu mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.  Profesa Joyce Ndalichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alipotembelea mradi huo mapema jana. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.  Prof.  Joyce Ndalichako

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa mabweni ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.  Profesa Joyce Ndalichako na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
 (Picha Na: Lilian Lundo)
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania