CURRENT NEWS

Monday, September 12, 2016

SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA YAWAONDOA HOFU WAZAZI

Mhitihimu  wa darasa la  saba  shule ya  Southern Highlands Mafinga akipongezwa na mama yake mzazi mwalimu Makanja
Mwanafunzi  aliyeongoza masomo yote Rahma Mdeka akipokea cheti cha kuhitimu darasa la  saba na zawadi yake  wakati wa mahafali ya  shule ya  Southern Highlands Mafinga
Mwanafunzi  aliyeongoza masomo yote Rahma Mdeka akipokea cheti cha kuhitimu darasa la  saba na zawadi yake  wakati wa mahafali ya  shule ya  Southern Highlands Mafinga
 Mkurugenzi wa shule za Southern Highlands Mafinga ,Mary  Mungai  kulia akitambulisha watumishi  wa  shule  hiyo.
........................................
Na MatukiodaimaBlog
UONGOZI  wa  shule ya  Southern Highlands Mafinga  wilayani  Mufindi umewataka   wazazi  wa  wanafunzi zaidi ya 50 waliofanya mtihani wa Taifa  wa darasa la  saba katika shule   hiyo  kuanza  kuwa na uhakika  wa watoto wao  kufaulu mtihani   huo .

Huku  ukiahidi  kutoa kuchangia sehemu ya ada kwa  wanafunzi watakajiunga na shule ya sekondari  ya  Southern Highlands Mafinga kama  sehemu ya ahsante kwa  ushirikiano  ambao  wazazi  wamekuwa  wakitoa kwa shule   hizo.

Mkurugenzi mtendaji wa Southern Highlands Mafinga  Mary  Mungai  aliyasema haya jana  wakati wa mahafali ya darasa  la  saba  shuleni  hapo .


"Shule hii ilianza mwaka 1994 kama day care na pre-school. Mwaka 1997 ikakuwa na
kuanza shule ya msingi-primary school.....mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza
wa darasa la saba wanafunzi walikuwa 17,wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa
kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza Katika matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 southern highlands
school ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya somo la kiingereza "


Alisema  kuwa matokeo mazuri ya wanafunzi wote kufaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba yamekuwa ni kawaida  kwa  shule   hiyo na  kuwa  toka  kuanzishwa kwake haijapa pata  kufelisha hata  mwanafunzi  mmoja .


Hivyo  kuwataka  wazazi  kutokuwa na hofu  juu ya  wanafunzi hao  waliofanya mtihani mwaka  huu kwani waanze  kujiandaa kwa kuwapeleka  sekondari.

Wakati  huo   huo mkurugenzi wa familia  ya Lucy Chawe inayoishi nchini marekani na Tanzania  imepongeza jitihada za  shule  hiyo na  kuahidi  kuendelea  kuiunga mkono  serikali kwa  kuhamasisha masomo ya Sayansi na Hisabati kwa  wanafunzi .

Mkurugenzi  wa The Chawe Foundation Award , Kitove Mungai  alisema  kuwa  kila mwaka  wamekuwa wakitoa  zwadi kwa  wanafunzi wa Awali   hadi  darasa la  saba ambao wamekuwa  wakifanya vizuri masomo ya  Hisabati na  sayansi .

Aliwataja   wanafunzi  ambao  wamepewa  zawadi hiyo kwa mwaka  huu kuwa ni Brayan Mgomapayo, Rahma Mdeka na Ayub Toss ambao  walifanya  vizuri katika hesabu .

Wakati katika  sayansi wanafunzi waliopewa  zawadi ni  Nimrod Nyakunga , Rahma Mdeka na Erick Mwanjelwa .


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania