CURRENT NEWS

Thursday, September 22, 2016

TUNDURU YAKABIDHIWA OFISI YA MADINI

Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini,Wasanifu majengo pamoja na Wakandarasi waliojenga jengo la ofisi ya Madini Mkazi Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la ofisisi ya madini Tunduru.mstari wa mbele kutoka kulia ,Msanifu majengo wa SMMRP, Joseph Ringo, mkurugenzi msadizi rasilimali watu,joyceline lugora,mkuu wa Kitengo cha Tehama Fransince Fungameza,Mkuu wa Kanda ya Ziwa Nyasa Kamishna Msaidizi wa Madini ,Mhandisi Fedy Mahobe.
Msanifu Majengo wa SMMRP , Joseph Ringo akitia saini hati za makabidhiano ya jengo la ofisi ya Madini  Mkazi Wilani Tunduru mkoani Ruvuma,( kulia) akishuhudiwa na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Nyasa,  Mhandisi Fred Mahobe( wa pili kulia)
Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali watu  wa Wizara ya Nishati na Madini Joyceline Lugora (  mstari wa mbele wa pili kushoto) akikabidhi ufunguo wa jengo la ofisi ya Madini  Mkazi Wilani Tunduru mkoani Ruvuma, kwa Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Nyasa,  Mhandisi Fred Mahobe,( mstari wa mbele wa pili kulia) mara baada ya kukabidhiwa kutoka  kiongozi wa timu ya ushauri ya ujenzi wa jengo hilo, Msanifu Majengo Paul Mshana (kushoto katikati) aliyepewa dhamana ya kusimamia ujenzi wa jengo hilo.Taswira tofauti za muonekano wa jengo la Ofisi ya Madini Mkazi  wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, jengo hilo limejengwa na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini
 ( SMMRP) unaotekelezwa na Benki ya Dunia.
 Na Zuena Msuya, Tunduru ,RUVUMA,

Wizara ya Nishati na Madini, kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini(SMMRP) imepokea jengo la ofisi  ya Madini  Mkazi wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma kutoka kwa kampuni ya  ukandarasi ya  Mkongo Contractors  ili kuanza kutumika na ofisi hiyo baada ya kufanyiwa ukarabati .

Akizungumza mara baada ya kupokea jengo hilo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma hivi karibuni, Msanifu Majengo wa SMMRP , Joseph Ringo alisema kuwa lengo la kufanya ukarabati katika jengo hilo ni kuimarisha shughuli za kiutendaji katika uendelezaji wa shughuli za madini wilayani ya Tunduru na viunga vyake  ukizingatia kuwa wilaya hiyo imejikita zaidi katika uchimbaji wa madini ya vito vya aina mbalimbali.

 Aidha Msanifu majengo Ringo Alifafanua kuwa kama  ilivyo dhamira ya mradi wa SMMRP ,kufanyika kwa ukarabati katika jengo hilo kutawezesha Afisa Madini Mkazi wa eneo hilo kufanya kazi zake kwa ufanisi  na kufikia malengo aliojiwekea katika kuwahudumia wadau wa madini.

Vilevile alisema kuwa ukarabati wa jengo hilo umefadhiliwa na Serikali ya Tanzania  kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ambao umejumuisha vifaa vya kisasa ikiwemo kuunganishwa na mfumo mpya na wa kisasa wa TEHAMA ambao unarahisisha utunzani wa kumbukumbu za wadau wa madini tofauti na ilivyokuwa hapo awali. 

Kwa upande wake Ofisa Madini mkazi Tunduru, Mhandisi Fredrick Mwanjisi aliupongeza mradi wa SMMRP kwa kuboresha na kuzijengea uwezo ofisi za madini nchini ili kuboresha shughuli za uendelezaji wa rasilimali za madini.

Hata hivyo Mhandisi Mwanjisi ameushauri mradi wa SMMRP,kutumia muda mfupi katika kutekeleza shughuli zake za ukarabati na ujenzi wa majengo mbalimbali kwa lengo la kuendeleza rasilimali madini.

Naye Mkurugenzi Msaidizi rasilimali watu wa Wizara ya Nishati na Madini,Joyceline Lugora, amewataka maafisa madini wakazi na wakanda zote nchini kutunza miundombinu ya majengo hayo ili kuondoa gharama za ukarabati wa mara kwa mara.


Na pia ichukue muda mfupi kukarabati eneo lililoharibika endapo kumetokea uharibufu katika jengo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania