CURRENT NEWS

Thursday, September 22, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMETOA SIKU 14 KWA WANAOMILIKI VIWANJA BILA KUVIENDELEZA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi  Evarest Ndikilo baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania Septemba 21, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman  baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania Septemba 21, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge  Dkt, Tulia Ackson baada ya kuwasili kwenye eneo inapojenjwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kuzindua Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania Septemba 21, 2016. 

 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo akizungumza  katika   uzinduzi  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji  akizungumza katika   uzinduzi  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.

 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird  akizungumza katika   uzinduzi  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016. 
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akizungumza katika uzinduzi  katika   uzinduzi  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaidiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othaman kukata utepe wakati alipozindua  Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania  mjini Kibaha, Septemba 21, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha   Mpango Mkakati na Mradi wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania  baada ya kuuzindua mjini Kibaha, Septemba 21, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Dkt. Hassison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria, Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande na Naibu Spika wa Bunge, Dkt Ackson Tulia.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa Nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird kitabu cha Mradi wa Maboresho  ya Huduma za Mahakama ya Tanzania  baada ya kuuzindua mjini Kibaha Septemba 21, 2016. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman  na kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani na Mahakama ya Wilaya ya Kibaha  Sptemba 21, 2016.
 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya  pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa  Mpango Mkakati na Mradi  wa Maboresho ya Huduma za Mahakama ya Tanzania ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Kibaha Septemba 21, 2016.
 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiondoka baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la Hakimu Mkazi Mahakama ya Pwani na Mahakama ya wilaya ya Kibaha Septemba 21, 2016. Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia, Bella Bird (kulia kwake) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (kulia) baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo la Hakimu Mkazi Mahakama ya Pwani na Mahakama ya wilaya ya Kibaha Septemba 21,2016. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.

 (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)
Na. Sheila Simba-MAELEZO
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku 14 kwa taasisi za serikali zinazomiliki viwanja bila kuviendeleza mkoani Pwani viwanja kuanza mara moja hatua ya kuendeleza  maeneo yao.

Aliyasema hayo leo Kibaha Mkoani Pwani wakati alipokuwa akizundua uzinduzi mpango mkakati (2015-20) na mradi wa maboresho ya huduma za mahakama nchini.

Amezitaja taasisi za umma zinazomiliki viwanja hivyo ni Wizara ya fedha, Njuweni Institute, Chuo kikuu Huria, Shirika la umeme nchini (Tanesco)  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

“Taasisi hizi ziandikie barua na waseme lini wataviendeleza viwanja hivi mpaka mwezi wa sita 2018 na waanze mara moja ujenzi viwanja hivyo baada ya hapo vitarudishwa kwa mkoa na tutawapa watu wengine”,alisema Majaliwa

Aidha,alisema Waziri mkuu aliipongeza mahakama kwa mpango wake huo wa kuendeleza na kujenga majengo ya mahakama nchini wenye lengo la kumsaidia mwananchi wa kawaida kupata huduma za mahakama kwa urahisi.

Majaliwa alisema kuwa mahakama nichini zinatakiwa kuzingatia kutenda haki kwa watu wote bila kujali hali ya mtu,kijamii au kiuchumi na kutochelewesha haki bila sababu za msingi.

Aliongeza kuwa mahakama inapaswa kutoa fidia ipasavyo kwa watu walioathirika kutokana na makosa ya watu wengine kwa mujibu wa sheria.

“lengo la mhimili huu ni kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwapunguzia umbali wanaotembea kufuata huduma na unalenga kupunguza muda wa mashauri kukaa mahakamani”alisema Waziri Mkuu Majaliwa

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande alisema mpango mkakati wa mahakama nchini ni dira na muelekeo wa kufikia lengo la kuwa na karibu na wananchi na kutoa huduma za utoaji haki.

Ameeleza kuwa mahakama imejipanga kufika malengo ya dira ya maendeleo 2025 ya kufikisha nchi kwenye uchumi wa kati kwa kutekeleza uadilifu, usawa, ushirikiano, weledi, uwajibikaji na uwazi.
Jaji Mkuu Chande ametaja malengo waliojiwekea mahakama ni utawala bora,uwajibikaji, usimamizi wa rasilimali, upatikanaji na utoaji wa haki kwa wakati na kuimarisha imani ya jamii na ushirikishaji wa wadau katika shughuli za mahakama.

“Tunachofanya sasa ni kuboresha miundombinu ya mahakama mijini na vijijini, kuongeza fursa ya upatikaji wa haki kwa makundi maalum ya wahitaji na kubadilisha tawsira ya mahakama” alisema Jaji Mkuu

Jaji Mkuu Othuman Chande,mahakama imefanikiwa ndani ya miaka 3 kufika lengo la kuwa na asilimia  80 ya mashauri ukilinganisha na miaka 3 ya nyuma wakati asilimia 80 ya mashauri yalikuwa ni yale ya miaka 5 na miaka 20.

Alieleza kuwa kwa kipindi cha mwaka 2016 2017 wanamalengo ya kimkakati ya kuondokana na mashauri yote yenye zaidi ya miezi mitatu hadi sita kwa mahakama za mwanzo,wilaya na hakimu mkazi.

Naye mwakilishi mkazi wa benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird alisema wameikopesha serikali Tsh 141 Bilioni ili kusaidia katika kuboresha huduma za mahakama kutokana na umuhimu wake katika kutoa haki kwa jamii ya kitanzania.

uzinduzi huo wa mpango mkakati na mradi wa maboresho ya huduma za mahakama nchini uliambatana na kuzindua jengo la mahakama ya hakimu mkazi pwani wilaya ya kibaha lilojengwa na chuo kikuu cha ardhi nchini  na kuweka jiwe msingi.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania