![]() |
Mtafiti na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja |
Na Sheila Simba,Maelezo
Serikali meshauriwa
kusimamia uwekezaji katika sekta za
kilimo,madini na viwanda ili kufikia malengo waliojiwekea ya kuwa na uchumi wa
viwanda ifikapo 2025.
Wito huo umetolewa na Mtafiti
na mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja
katika mahojiano na MAELEZO kuhusu hali ya uchumi nchini katika kufikia uchumi
wa kati kupitia viwanda.
“Muhimu sasa Serikali
kuwekeza zaidi katika sekta ya Madini,kilimo na viwanda na hili litasaidia
kufanya nchi kuzalisha bidhaa zitakazouzwa nchini kwa wingi bila kutengemea
bidhaa kutoka nje ya nchi”,alisema Prof.Semboja.
Ameeleza kuwa taarifa
ya hali ya uchumi iliyotolewa na Benki Kuu nchini imeweka wazi hali ilivyo kwa
sasa,na kuongeza kuwa ni kweli uchumi upo imara kutokana na taarifa
zilizokusanywa na Benki hiyo kutoka vyanzo
mbali mbali.
“Ni kweli kwamba uchumi
wetu upo imara na kwamba uchumi wetu unapimwa kwa kuangalia vigezo vinne ambavyo ni pato la taifa,mfumuko wa bei,urari wa
biashara na upungufu wa fedha serikalini”,alisema Prof. Semboja.
Aidha,Prof Semboja
amesema kuwa serikali kwa sasa imepunguza matumizi ya fedha yasiyo ya lazima na
imeongeza makusanyo ya kodi kutoka vyanzo mbalimbali.
“Serikali haina
matumizi makubwa ya fedha kwani matumizi yanendana na mapato yanayokusanywa ”,alisema
Semboja
Amesema kuwa wanaolalamikia
kutoonekana kwa fedha mtaani ni wale waliokuwa wanapata pesa kwa njia ambazo
sio halali na hivyo kupelekea kushindwa kupata kwa sasa kutokana na udhibiti
uliwekwa na Serikali katika kukusanya na kusimamia kodi kwa utaratibu halali.
Ameongeza kuwa Serikali
fedha inazokusanya zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote na sio kwa wachache
waliokuwa wakijinufaisha wenyewe.
MWISHO.
Post a Comment