CURRENT NEWS

Saturday, October 15, 2016

DC KILOLO ATAKA ASASI YA LASWA KUSAIDIA KUKOMESHA MIMBA ZA UTOTONI

Mkurugenzi wa  asasi  ya msaada  wa  kisheria  ya  LASWA mkoa  wa Iringa Francis Mwilafi  akizungumza  wakati wa uzinduzi wawa mradi wa  kuimarisha huduma ya  wasaidizi  wa   kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji  wa haki  kwa  wote  hasa  akina mama wajawazito na  watoto,warsha  iliyoshirikisha madiwani na watendaji  wote  wa kata  za  wilaya ya  Kilolo ,kulia ni meneja wa LASWA Oscar Lawa
Katibu  tawala wa wilaya ya  Kilolo Yusuph Msawanga  akizindua   wa mradi wa  kuimarisha huduma ya  wasaidizi  wa   kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji  wa haki  kwa  wote  hasa  akina mama wajawazito na  watoto

Madiwani  wa Halmashauri ya  Kilolo  wakiwa katika  picha ya pamoja na mgeni rasmi katibu tawala wa Kilolo Yusuph Msawanga  wa  nne  kutoka  kulia mara  baada ya uzinduzi  wa mradi wa  kuimarisha huduma ya  wasaidizi  wa   kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji  wa haki  kwa  wote  hasa  akina mama wajawazito na  watoto
Mkurugenzi wa Laswa  akieleza  lengo la mradi  huo
Watendaji wa kata  zote za Kilolo  wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi  katibu tawala wilaya ya  Kilolo

Katibu  tawala  wa wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa Yusuph Msawanga  (wa  nne kulia waliokaa) akiwa na mkurugenzi  wa asasi  isiyo ya  kiserikali inayojihusisha na huduma ya msaada wa  kisheria  wa bure kwa  wananchi mkoani Iringa Francis Mwilafi kushoto  kwake na baadhi ya  wafanykazi wa  LASWA na madiwani mara  baada ya uzinduzi  wa mradi wa  kuimarisha huduma ya  wasaidizi  wa   kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji  wa haki  kwa  wote  hasa  akina mama wajawazito na  watoto


Na MatukiodaimaBlog 

MKUU  wa  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa  Asia Abdalah ameiomba  asasi  iyoso  ya  kiserikali  inayojihusisha na  msaada  wa  kisheria ya LASWA   kusaidia  kutoa  elimu zaidi  kwa wananchi  ili   kuwezesha jamii  wilayani  humo kujua  sheria na  kukomesha mimba  za utotoni na unyanyasaji kwa wanawake .

Akizungumza katika  uzinduzi  wa mradi wa  kuimarisha huduma ya  wasaidizi  wa   kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji  wa haki  kwa  wote  hasa  akina mama wajawazito na  watoto , jana mkuu huyo aliyewakilishwa na katibu tawala  wa  wilaya   hiyo Yusuph Msawanga  alisema  kuwa mradi  kuzinduliwa kwa mradi huo katika  wilaya   ya Kilolo iwe ni mwisho wa jamii  kunyanyasika na iwe  mwisho wa mimba za utotoni .

Alisema  kuwa jamii kutokana na kutojua  sheria ama  wajibu  wao  kwa  watoto kumekuwepo na changamoto  za watoto  wa  kike  kukatishwa masomo  yao  kutokana na mimba  za  utotoni ama  wato  kuwatorosha  kwenda  kufanya kazi jambo  ambalo kisheria  ni  kosa .

Hivyo  alisema  kutokana na mafunzo hayo yametolewa kwa  madiwani na  watendaji wa kata  zote za  wilaya  ya  Kilolo na LASWA  kutoa wasaidizi wa  kisheria kwa  kila kata  ni uwazi  kuwa jamii  itaelimishwa juu ya  sheria  mbali mbali na hata  kuwezesha changamoto  za  mimba  za utotoni na  wajane kunyanyasika kwa  kutojua haki zao  kupungua  zaidi.

" Nawaombeni sana   washiriki  wa mafunzo haya ambao ni madiwani na  watendaji wa kata  tumieni mafunzo haya kusaidia  jamii kuepukana na unyanyasaji  wa aina mbali  mbali  ikiwa ni  pamoja na kupambana na  wale  wanaokwamisha  watoto wa  kike  kuendelea na masomo kwa kuwapa mimba ....ila kwa  LASWA naomba  sana  mzidi  kutoa mafunzo haya kwa makatibu tafara ikiwezekana hata kwa  watendaji wa  vijiji ili   elimu  hii iwafikie  watu  wengi  zaidi"

 Kuhusu  wasaidizi  wa  kisheria wa LASWA  waliopo katika ofisi za  watendaji ngazi ya kata alisema  kuwa ni vizuri  kila mmoja  kufanya kazi yake kwa  kusaidia jamii na  kuepuka  kutumika kukandamiza  watu  wasiojua  sheria

Kuwa  iwapo  wasaidizi hao  watasaidia  kutoa  elimu ya msaada wa  kisheria kwa  wananchi  wenye uhitaji  upo  uwezekano mkubwa wa  jamii wilayani  humo  kujikita  zaidi katika  uzalishaji mali badala ya  kupoteza  pesa  nyingi  kwenda  kutumia katika kesi mahakamani .Meneja  wa LASWA  Oscar Lawa  alisema  kuwa   kuwa  mafunzo  hayo yameandaliwa na asasi  yake ya LASWA Iringa   kwa  ufadhili wa LSF ya  jijini Dar es  salaam kwa  chini  ya  ubalozi  wa Denmark   kuwa  sifa  ya  msaidizi  wa  kisheria ni  kuwa na akili timamu  pia  sifa ya kuheshimu na  kulinda  sheria za mbali  mbali  za nchi na haki za  binadamu
Mkurugenzi   huyo  alisema hadi  sasa  wamekwisha  toa mafunzo  na  kuwa na vijana katika  wilaya zote tatu  za  mkoa  wa Iringa  ikiwemo ya  Kilolo, Mufindi na Iringa kwa kuwa na vijana wasaidizi wa  kisheria
Aidha  alisema faida  kubwa ya  msaidizi wa  kisheria  ni kupunguza na kuziba pengo  la ukosefu wa huduma za msaada  wa kisheria katika jamii anayoishi  kwa  kutoa usaidizi wa  awali wa kisheria.


Hata  hivyo  alisema  lengo  kuu la mradi huo  ni  kufanya wasaidizi  wa  kisheria (Paralegals)   kujengeka  kiuwezo  na  wafahamike katika  jamii  wanazoishi  na kuwawezesha  kuwafikia kiurahisi   wahitaji katika maeneo yao .

 Ili  kuwezesha  kufikiwa kwa  lengo hili  la mradi  unahitaji  ushirikiano  wa  kutosha   kutoka kwa  viongozi wa  serikali  kuanzia ngazi ya  kitongoji hadi  ngazi ya  wilaya  na kuwa wasaidizi hao wa kisheria  bila  kupata  ushirikiano  kutoka kwa madiwani  na  viongozi  wote  wa ngazi ya kijiji hadi wilaya  kwani  pasipo hivyo wananchi watacheleweshwa  kupata haki  yao.

"Muda  wa  utekelezaji wa mradi  huu ni miaka minne  kwa gharama  ya milioni 100 ambapo vituo  vya  wasaidizi wa  kisheria watalipiwa pango la ofisi  na kupewa nauli ya kuwafikia  wahitaji wa  huduma ya bure ya kisheria maeneo mbali mbali  pia  kutumika  kufikisha elimu ya kisheria  mfano katika mikutano ya hadhara  ,mabaraza ya  maendeleo ya kata  kila mwaka kituo  cha msaada wa  kisheria  kitapewa  Tsh  milioni 8 za  uendeshaji "

Huku  mkurugenzi  mkuu  wa LASWA  Iringa  Francis Mwilafi  pamoja na  kuwapongeza washiriki wa  warsha hiyo na uongozi wa wilaya ya  Kilolo kuutambua mradi  huo bado  alitaka  viongozi  wote wa  serikali na madiwani  kutoa ushirikiano mkubwa kwa wasaidizi hao  wa kisheria ili  kuwezesha  jamii  kuweza  kunufaika na mradi huo .


Mwilafi  alisema  kumekuwepo na mafanikio makubwa  ya  mradi huo kwani hadi  sasa LASWA  mkoa  wa Iringa  imefanikiwa  kuweka msaidizi wa  kisheria  kwa  kila kata ya wilaya  zote za mkoa  wa Iringa.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania