CURRENT NEWS

Friday, October 14, 2016

HAYA NDIO YATAKAYOJIRI LEO WILAYA YA CHEMBAKatika kuazimisha kumbukizi ya miaka 17 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere, Maadhimisho ya kilele cha wiki ya Vijana pamoja na Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru hapo  leo tarehe 14/10/2016. Wilaya ya Chemba imepanga kufanya yafuatayo katika kuenzi harakati na juhudi za Muasisi huyu wa Taifa letu.

Ikumbukwe Mwl Nyerere katika maisha yake alipigania ukombozi wa Tanzania katika 1. Kupambana na adui ujinga. 2. Adui Maradhi. 3. Adui Umasikini na 4. Adui njaa.

Hivyo Wilaya yetu itaadhimisha siku hii kwa kushiriki kwa kusafisha eneo itakapojengwa Zahanati ya Kijiji cha Chemba katika Wilaya ya Chemba na wananchi watachangia matofali ya ujenzi wa Zahanati hiyo. Vile vile zoezi hilo litaendana na uchangiaji wa damu katika benki ya damu hapa Wilayani Chemba.

Baadae Kutakuwa na Michezo ya kuvuta kamba  baina ya Watumishi wa Serikali na Wananchi wa Kijiji cha Chemba.

Kukimbiza kuku na mwisho kutakuwa na mchezo wa bao kati ya Wazee wa hapa Chemba katika kumuenzi Mwl Nyerere ambaye alikuwa mpenzi mkubwa wa mchezo huu.

Washindi katika mchezo wa kuvuta kamba na nao watajinyakulia zawadi ya Mbuzi na ule wa kukimbiza kuku kwa upande wa wanawake na wanaume watajinyakulia kuku watakaye mkamata.

Hivyo Katibu Tawala wamewaomba wananchi wa Chemba na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi bila kukosa katika tukio hili la kipekee la kuenzi juhudi za Baba wa Taifa katika kuwaletea wananchi maendeleo majira ya saa 2:00 asubuhi ya leo katika viwanja vya michezo shule ya Msingi Chemba.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania