Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Selemani Jafo akiwa na baadhi ya viongozi wa Babati akiwemo Mbunge wa Babati vijijini Jitu son pamoja na Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymond Mushi.
Naibu Waziri wan chi,
Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Selemani Jafo, akiongea na
kina mama wajawazito wanaosubiria kujifungua katika jengo maalum kwa kinamama
wanaotoka mbali ili kuepuka vifo vya kinamama wakati wa kujifungua katika
hospitali ya Iramba, Singida.
......................................................
NAIBU Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo
amekemea tabia iliyokuwa ikifanywa awali na baadhi wa watumishi wasio waadilifu
kwa kuchukua rushwa kwa wakandarasi wa miradi ya ujenzi kwa kuwalazimisha kutoa
fedha ili kupewa kazi na kuidhinishiwa malipo yao.
Jafo alisema kwamba
kumekuwa na tabia ya "Utatu usio mtakatifu " katika halmashauri ambo
una athiri sana utekelezaji wa miradi ya ujenzi.
Utatu huo unawahusisha
Afisa Manunuzi, Mhandisi wa ujenzi, na mweka Hazina (DT), ambapo Jafo alisema
kwamba halmashauri ikiwa na kazi ya ujenzi Afisa Manunuzi anaweza mazingira
kupata fedha ili mkandarasi apewe kazi.
Mkandarasi akishapata kazi
anakutana na kizingiti kingine kutoka kwa Mhandisi (Engineer) ambaye anagoma
kupitisha certificate yeyote ya kazi iliyofanyika mpaka apewe chake mapema.
Kizingiti cha tatu kinajitokeza pale Mweka
Hazina (DT) kugoma kuandaa malipo na kutoa cheki ya mkandarasi hadi apewe
chake. Haki hii inamfanya Mkandarasi wa ujenzi anajikuta ametoa fedha
nyingi ili apate kazi na kupokea malipo.
Kutokana na Utatu huo, umesababisha baadhi ya
miradi kujengwa chini ya kiwango hivyo kuharibika baada ya kipindi kifupi.
Jafo alikemea tabia hiyo alipokuwa
akikagua miradi ya maendele na kuongea na watumishi wa halmashauri za wilaya ya
Babati, Mbulu, Nzega, Igunga na Iramba.
Aliwataka wafanyakazi wa
halmashauri kufanya kazi kwa kujiamini na kuzingatia kanuni za utumishi wa
umma.
Aliwaagiza wakurugenzi
kukuza vipaji vya watendaji wao kwani wengi wao japo ni wasomi wazuri lakini
wamekuwa hawatumiki vyema na baadhi yao kutopewa kipaumbele katika idara zao.
Post a Comment