CURRENT NEWS

Tuesday, October 4, 2016

LUKUVI AKABIDHI BATI 2000 NA POWER TILA KWA MADIWANI WAKE WOTE JIMBO LA ISMANI

Katibu wa mbunge  jimbo la Isimani Bw  Thom Malenga  kulia akimkabidhi  diwani wa Mboliboli Khalfan Lulimi msaada  wa bati kwa  ajili ya  kukamilisha ujenzi wa  miradi ya maendeleo katani kwake  msaada  huo umetolewa na mbunge  Wiliam Lukuvi kwa kata  mbali mbali kwa kutoa bati 2000 zenye  thamani ya  Tsh milioni 44 na Power tila 15 kwa madiwani  wote wa CCM jimboni mwake
Diwani wa Mlolo  Charles  Nyagawa kushoto akikabidhiwa  bati na katibu wa mbunge wa Isimani Thom Malenga
Madiwani  wakipokea  bati
Diwani wa viti maalum Idodi  Sophin Msekwa  akipokea  msaada wa badi
Diwani wa Mlenga  akipokea  bati
; Diwani wa kata ya Malenga makali  Flanzisca Kalinga akiwa akijiandaa kuendesha moja kati ya  Power tila 15 zenye  thamani ya  Tsh milioni 105   zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa  Wiliam Lukuvi kwa  ajili ya madiwani  wote 15  wa CCM jimboni mwake kama miradi yao pamoja na bati 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo jimboni humu wa tatu  kushoto ni katibu wa mbunge Lukuvi , Thom Malenga ambae  alikabidhi kwa niaba ya mbunge  Lukuvi akiwa na baadhi ya madiwani  hao

Na MatukiodaimaBlog 
MBUNGE  wa  jimbo la  Isimani Wiliam Lukuvi  aametoa  msaada  wa  bati  2000   ajili ya  kukamilisha  miradi  ya  kimaendeleo katika kata  mbali mbali  za  jimbo  hilo pamoja na  kuwasaidia madiwani  wote 15   wa  chama  cha mapinduzi (CCM)  Power Tila vyote  vikiwa na thamani ya zaidi ya  Tsh milioni 100.44

Lukuvi  alisema amelazimika  kukabidhi msaada  huo wa power tila kwa madiwani  wake  ili  kuwawezesha  kiuchumi  pia  kusaidia  kusukuma maendeleo katika kata  zao kama  kuwasaidia  wananchi  kutumia power tila hizo kuendeshea  shughuli mbali mbali za  kijamii zikiwemo   za  kilimo.

Kwani  alisema kuwa power Tila   hizo  amezinunua zikiwa na  kamili ya  vifaa vyake  vyote kama jembe la  kulimia pamoja na tela zake kwa  ajili ya  kusafirishia  mazao ama kufanyia  shughuli  nyingine za  kijamii katika kata .

Akikabidhi  msaada  huo leo   kwa niaba ya  mbunge  Lukuvi katibu  wake Thom Malenga  alisema  kuwa  kuwa lengo la msaada  huo ni  kusukuma mbele  maendeleo ya  wananchi wa jimbo la Isimani na kuwa msaada wa bati  unakwenda katika  kata  zote  ambazo  zina miradi ya  ujenzi wa  shule ,nyumba  za walimu na  zahanati ambazo  zilikuwa  zikihitaji bati  ili  kumalizia  ujenzi   huo na  kuwa  bati  zote ziliotolewa ni 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44

Wakati msaada  huo wa power  Tila umeelekezwa kwa madiwani  15  wa CCM waliopo katika  jimbo  hilo na kuwa kila power tila moja imegharimu  kiasi cha  Tsh milioni 7 na kwa  powertila zote  zimegharimu  Tsh  milioni 105 lengo  kubwa la  kutoa msaada  huo ni kuwawezesha madiwani hao  kuwa na vitega  uchumi na  kuongeza ari ya  kuwatumikia  wananchi wao .

Hivyo  alisema  kuwa  kupitia msaada  huo wa bati anaamini madiwani hao  wakiwa ni  wenyeviti wa kamati za maendeleo  ya kata  kuhakikisha  wanasimamia  vema  miradi ya  ujenzi inayoendelea katika maeneo  yao na kwa upande wake mbunge ameamua  kutoa msaada  huo wa bati kama  njia ya  kuwapunguzia makali wananchi  wake  kwa ajili ya kuchangia pesa kununua bati   hizo.

" Mheshimiwa  mbunge  amewaunga mkono   wananchi  kwa kazi waliyoifanya ya  kusimamisha  kuta za  vyumba vya madarasa na zahanati na kwa ajili ya  kuwaunga mkono bati  amelazimika  kununua "

Hata  hivyo  alisema kwa upande wa power  Tila  hizo  alisema  ni mradi  binafsi wa madiwani  wake kwa  ajili ya  kuwasaidia  wananchi  wao hivyo kazi ya  diwani na  kusimamia shughuli za kimaendeleo na pale  wananchi  wanapohitaji msaada wa power tila hizo basi  mwenye  mamlaka  nazo ni  diwani  mwenyewe na  sio mradi wa kata  wala kijiji .

Makamu  mwenyekiti wa Halmashauri ya  Iringa na diwani wa kata ya Mboliboli Khlfani Lulimi  akishukuru kwa niaba ya madiwani  wenzake  alisema  kuwa  msaada  huo ni mkubwa kwao na zaidi wanampongeza mbunge  wao kwa  kuthamini kazi  inayofanywa na madiwani na  kuwa watahakikisha power tila hizo zinaleta chachu ya maendeleo katika maeneo yao.


Wakati  diwani  wa kata ya Malenga Makali FLanzisca  Kalinga na diwani wa viti maalum tarafa ya Idodi  Sophin Msekwa   pamoja na kupongeza msaada  huo  walisema  wanategemea kutumia power tila hizo kwa ajili ya  kuwasaidia wanawake na watoto hasa  ukizingatia  kuwa kumwezesha mwanamke ni kuisaidia jamii nzima.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania