CURRENT NEWS

Sunday, October 23, 2016

RIDHIWANI:VIJANA MSHIKE SANA ELIMU KWANI NDIO MKOMBOZI WENU

Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete akizungumza katika maafali ya shule ya Sekondari Chalinze  wa upande  kulia  ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Bwilingu Ndg. Nassar Tamim.

Diwani wa kata ya Bwilingu Ndg. Lucas Lufunga akizungumza neno la utangulizi kabla ya kumakaribisha mgeni rasmi Mbunge wa jimbo  la Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete kuzungumza na wananchi wa Bwilingu kwenye mahafali shule ya sekondari Chalinze

Mgeni rasmi Mh.Ridhiwani Kikwete akimpongeza mwanafunzi Athumani Mwalimu aliyefanya vizuri katika upande wa taaluma kwa kupata alama ya A katika masomo yote kwenye mtihani wa majaribio(moko) 

Mwalimu Godwin akipongezwa kwa kusimamia vizuri wanafunzi shuleni hapo. na mgeni rasmi ambaye ni Mbunge  wa Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete.

Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Chalinze akiweka msisitizo katika suala la maadili mema kwa vijana na kuhakikisha kuwa wanafaulu vizuri ili kuendelea kuipa hadhi na heshima shule ya Chalinze
Wito umetolewa kwa vijana nchini kusoma kwa bidii na kuwekeza katika elimu ili kuweza kujikomboa na kufanikiwa katika maisha yao ya badae.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete katika maafali ya shule ya sekondari Chalinze,na kuwaasa vijana kushikamana na elimu kwani ndio mkombozi wao katika maisha.

“ili ufanikiwe katika maisha ni lazima kuweka bidii katika masomo na kuachana na mambo yasiyo na tija katika kipindi hiki cha masomo”,alisema Ridhiwani

Aidha Mbunge huyo amewaasa vijana kutojiingiza katika makundi yasiyofaa katika jamii na kuongeza kuwa wapo wengi walioharibikiwa kwa kuingia katika makundi mabaya.

"Wako waliofanikiwa kwa kutumia vizuri elimu na  kuwa mfano bora kwa wengine bado mna safari ndefu jifunzeni kutoka kwa waliofanikiwa  ”,alisema Ridhiwani

Aidha Mbunge Ridhiwani alitumia nafasi hiyo kumpongeza kijana Athumani Mwalimu aliyefanya vizuri katika mitihani yake ya majaribio kwa kupata alama ya A katika masomo yake yote.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania