CURRENT NEWS

Friday, October 7, 2016

RUSIA: TUMEJIANDAA KUPAMBANA KWA AINA YOYOTE NA MAREKANI NCHINI SYRIABalozi wa Russia nchini Lebanon ametangaza kuwa tayari Moscow kukabiliana na chokochoko zozote za Marekani nchini Syria.

Alexander Zasypkin ameyasema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na gazeti la Lebanon la al-Jamhuriyyah ambapo sanjari na kuashiria juu ya kuwekwa ngao ya makombora ya S 300 katika mji wa bandari wa Tartus kaskazini magharibi mwa Syria, amesema kuwa, baada ya uamuzi wa Marekani wa kusimamishwa makubaliano na Russia kuhusiana na Syria, Moscow ilichukua hatua ya kujiimarisha zaidi kukabiliana na chokochoko tarajiwa ya Marekani ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Zasypkin ameongeza kuwa, Russia inashirikiana na serikali halali ya Syria katika kupambana na makundi ya kigaidi, kuboresha hali ya kibinaadamu, kuendeleza mchakato wa maridhiano na mazungumzo yenye lengo la kutatuliwa mgogoro wa nchi hiyo kwa njia za amani.
Balozi wa Russia nchini Lebanon amekosoa vikali siasa za undumakuwili za Marekani kuhusiana na magaidi na kuongeza kuwa, Washington haichukui hatua zozote za kukabiliana na makundi hayo na badala yake inafanya kila iwezalo kwa ajili ya kulimaliza jeshi la serikali ya Damascus.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania